Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 24, 2021

THE GUNNERS NDONDO CUP. KICHUYA NA WENZAKE WAIANGAMIZA TIMU YAO YA MORO KIDS.

Mshambuliaji hatari wa Salange Gamba ldd Marko[kulia] ambaye anacheza soka la kulipwa Uarabuni akimiliki Mpra kwenye juzi kwenye Michuano ya Ndondo Cup
Kipa wa Mprp Kids akiramba udogo baada ya kufungwa bao la kwanza na Gamba
Tajiri Abdallah Al -Saed akiwa kwenye benchi la Salange Fc huku akitabasau baada ya kushuhudia akipigwa Picha na Mwandishi wa Mtandao huu

Winga wa Salange Buja Kanyama akichungwa na Beki wa Moro Kids, Kamanya ni mchezji wa Moro Kids aliyetimmia Salange kwa kufuata maslahi bora
Winga wa Moro Kids Teps Evance ambaye pia anakipiga lhefu ya Mbeya alifunga bao la kwanza kwenye gemu hiyo
Winga wa Salange Shiza Kichuya ambaye kwa sasa anakipiga Namungo ya Lindim Mara baada ya ligi zote duniani kutamatika wachezaji wengi wamerejea majumbani kwao
                                            ....Kichuya Kona

...Teps wa Moro Kids akimgadi Shiza Kichuya aliyepiga Kona

                     ....Goooooo bao la Pili kwa Salange Fc
...Kipa wa Moro Kids akichika nyavu kwa uchungu baada ya kupigwa bao la pili
Kocha wa Moro Kids Salim Mbonde akiwapa maelekezo wachezaji wake wakati wa Mapunziko juzi. Bonde mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa alitema Simba baada ya kupata majeraha, awari kabla ya kujiunga na Simba  Ponde alitokea Moro Kids akaenda Mtibwa kisha akatimkia Simba
...Winga wa Moro Kids bo 12 mdomo umemponza baada ya kumbwatukia refa alilimwa kadi ya Njano
              ....Wachezaji wa Salange wakishangilia bao la 3
Mchezaji Gambo anayecheza soko la Kulibwa nchini Misri akitolewa nje baada ya kumia begam ahata hivyo baada ya gemu hiyo kutamatika Mtandao huu ulifanikiw akuzungumza na mchezaji huyo ambapo alisema baada ya kupatika huduma ya kwanza amepona kabisa

     Kocha Msaidizi wa Moro Kids akimpa maelekezo Tepsi
Mchezaji wa Moro Kids jezi namba 12 akilimwa kadi nyekundu'Umeme' baada ya kumkwatua kwa makusudi winga wa Salange Buja Kanyama
Mwananguuu. aliyekuwa kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Ally Jangalu mwenye Kapero akifuatilia gemu hiyo ya Moro Kids na Salange

 The Gunners Ndondo Cup si ya Mchezo mchezo Mshikakapendera bora wa ligi daraja la Kwanza Tanzania Bara Mkazi wa Mawenzi Morogoro Respicius Dismas juzi alikuwa line One robo fainali ya mwisho kati ya Salange Fc na Moro Kids.


 

                                                Na Dunstna Shekidele,Morogoro.

 

TIMU ya Matajiri wa Stend ya Msamvu ‘Salange Fc’ juzi walitinga nusu fainali ya Michuano ya The Gunners Ndondo Cup, baada ya kuitandika timu ngumu ya Moro Kids kwa bao 3-2.

 

Katika gemu hiyo ‘tamu’iliyojaa Vipaji na ufundi wa kira aina kwa muda wote wa dakika 90 imepigwa uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.

 

Hadi dakika 45 za awari zinakamilika Salange waliongozwa na Tajiri Abdallah Al-Saed ambaye ni Mjuu wa Tajiri wa Kampuni ya Mabasi ya Al-Sead walikuwa mbele kwa bao 3-0.

 

Huku Tajiri Al- Sead aliyeketi kwenye Benchi la Salange alipohojiwa na Mtandao huu kabla ya gemu hiyo kuanza alisema.

 

”Shekidele ni leo niko hapa kwa kazi moja tu nimewambia wachezaji mbali na Posho zao za mechi kila atakayefunga bao nitamlipa laki Moja kwa maana bao moja nitalinunua kwa laki Moja”alisema Al-Saed.

 

Kipindi cha Pili kilipoanza Kocha wa Moro Kids Salim Mbonde  beki wa zamani wa Simba ambaye pia chimbuko lake ni Moro Kids alifanya mabadiliko kwa kuwatoa baadhi ya wachezaji akiwemo Kipa kwa lengo la kuchomoa bao hizo 3.

 Mabadiliko hayo yaliza Matunda kwa Watoto wa Morogoro ’Moro Kids’ iliyoongozwa na Winga hata wa lhefu Teps Evance walifanikiwa kuwadhibiti Sangale na kufanikiwa kufunga bao 2 kufuati wachezaji wa Salange kukata Moto kama mchezo huo ungeongezwa kwa dakika 10 huenda Moro Kids wangechomoa na kufunga bao la 4.

 

Kama mchezo huo baadhi ya wachezaji wa zamani wa Moro Kids waliichezea Salange wakifuata Maslahi mazuri, wachezaji hao ni Shiza Kichuya ambaye kwa sasa anakipiga Namungo, Kipa Hashim Nzota aliyekuwa akiidakia Mji Njombe na Buja Kanyama ambaye hajatokabado yuko ndani ya taasisi ya Moro Kids.

Alipoulizwa kwa nini ameikacha timu yake akatimkia Salange, Kanyama alijibu kwa ufupi ‘Maslai kaka mashindano yakikamilika naludi timu yangu ya Moro Kids’.

 

Mbali na wachezaji hao Salange  ilimtumia pia beki wa Polisi Tanzania na Mshambuliaji wa kimataifa Mtanzania Mwana Morogoro  Gambo ldd Marko anaye Kipiga timu ya ligi kuu nchini Misri ya Azaifa huku yeye akitumikia timu B akipigania kupanda timu ya wakubwa.

 

 Katika mchezo huo Gamba alipiga bao 2 labla ya kutoka baada ya kumia bega,Mtandao huu utafanya mahojiano Maalumu  Clip Video na Gamba kuhusiana na ligi ya Uarabuni na ile ya hapa Tanzania sambamba na maisha yake kwa ujumla hivyo endelea kuwa jirani na Youtube ya Shekideleonlitv. Aidha Mtandao huu umezungumza na Winga wa lhefu Tepsi Mkazi wa Kilakala Morogoro kuhusiana na hatima yake kisoka kama atabaki lhefu iliyoshuka daraja au atarejea timu yake ya zamani ya Azam majibu ya maswali haya endelea kuwa jirani na Blog ya shekidele muda wote kwa habari za chini ya Kapeti.


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...