Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, July 27, 2021

BAADA YA GEMU YA SIMBA NA YANGA MWENYEKITI WA TAWI LA SIMBA ATINGA TAWI LA YANGA NA KUMVAA MWENYEKITI WA TAWI HILO.

Mwenyekiti wa Tawi kuu la Simba Mkoa wa Morogoro Maarufu tawi la Shujaa' Said Mkwinda akiwasili tawi la Yanga juzi mara baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mtani wake Yanga' a.k.a Wajukuu wa Mzee Mpili
 ....Mwenyekiti huyo wa Simba akimvaa Mwenyekiti wa tawi la Yanga lssa Kitukwa . Maarufu lssa Chabala'

Wenyeviti hao wakipozi mbele ya Kamera za Mtandao huu Mara baada ya kutaniana vya kutosha

Mwenyekiti wa tawi la Yanga  lssa ChabalaMwenye skafu ya Yanga shingoni, akilipa jeru  kwa muuza kahawa baada ya kumnunua Kahawa na Kashata Mwenyekiti wa Tawi la Simba Mkoani Morogoro Said Mkwinda'jezi nyekundu Pichani


 

                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MARA baada ya gemu ya watani wa Jadi Simba na yanga iliyopigwa juzi Mkoani Kogoma kutamatika kwa Simba kuinyuka Yanga bao 1-0.

Mwenyekiti wa tawi kuu la Simba Mkoa Morogoro Said Mkwinda ametinga tawi kuu la Yanga la Mkoani Morogoro na kumvaa Mwenyekiti wa Tawi hilo lssa Kitukwa ‘Maarufu lssa Chabala’huku akimtania kwa kichapo hicho.

Mwandishi wa habari hizi aliyekuwepo kwenye tawi hilo akisaka habari za chini ya Kapeti aliwatwanga Picha Viongozi hao ambao pia ni Marais wa Mitaa wanayoishi.

  Mwenyekiti wa Yanga’Chabala’ ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Fumilwa A Kata ya Mji Mpya  na Mwenyekiti wa Simba Mkwinda ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Simu B  kata ya Mji Mpya wote ni Makada wa CCM.

 Baada ya kupeana Maneno ya Utani wa Jadi Chabala alimnunua Kahawa Mtani wake Mkwinda huku akimueleza kwamba wakutana Ngao ya Hisani.

 Matawi hayo Makuu ya Simba na Yanga ya Mkoani Morogoro yapo Kata ya Mji Mpya jirani jirani yakitenganishwa na Mitaa 2 hivyo kila timu hizo zinapo cheza Moja akifungwa Mashabiki wa himu iliyoshinda utinga kwenye tawi la mtani wake na kumkera kwa maneno ya kejeri.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...