Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
MSANII Staa
wa nyimbo za lnjiri nchini Bahati Bukuku
amehubiri kupitia wimbo akisema ‘Dunia haina huruma’.
Kweli kuna
baadhi ya watu hapa duniani hawana huruma, wakati Mwandishi wa habari hizi akipambana
kusaka pesa za kumjengea nyumba Mohamed Matama ambaye ni Mlemavu wa Miguu.
Matapeli
wametumia fursa hiyo kumtapete mlemavu huyo elfu 50 alizopewa msaada na aliyekuwa kamanda
wa Polisi Mkoa wa Morogoro’RPC’ SACP Urlch Matei.
PICHA HILO LILIKUWA HIVI.
Mbali na
kuendesha harambee kwenye Mtandao Pendwa
wa Shekidele,Mwanahabari huyo pia alizungunza na Mlemavu huyo kwa viongozi na na
Mtajiri wa Mkoa wa Morogoro kuomba msaada.
Dunstana Shekidele na Matama walitinga Ofisi
wa RPC Matei Ghorofa ya kwanza kwa kuwa Ghorofa hilo halina lifti Mlemavu huyo
kwa Ujasiri alitambaa na kupanda ngazi mpaka juu ya ghorofa hilo.
Mungu
ambariki sana RPC Matei tulipofika tu ofisini kabla ya kumueleza shinda yetu
RPC huyo alisema
” Du huyu jamaa
kapandaje ngazi shekidele ungenipigia simu nije huko chini tuzungumze mbona
kuna ofisi nyingi kuliko kumpa adhabu ndugu yetu huyo ya kupanda huku”
Mwanahabri
huyo alimuomba msamaha ‘Big Bos’ huyo wa Polisi Mkoa Morogoro na Moja kwa Moja alimueleza shida za Mlemavu huyo ambapo RPC
Matei aliguswa na kumkabidhi Msaada wa elfu 50 huku akisema
“ Shekidele
ubarikiwe sana kwa kazi hii unayoifanya kwa sasa ninakiasi hichi kidogo naomba
mkipokee mwisho wa mwenzi nitachangia kiasi kingine “alisema RPC huyo.
Kabla hayatimiza
ahadi yake hiyo RPC Matei halihamishiwa Mkoa wa Mbeya, Mtandao huu unazidi
kumuombe baraka nyingi na wote
waliochangia ujenzi wa nyumba hiyo. UTAPELI SASA.
Matama ni
muunini wa dini ya kiislamu aliyejaliwa kuswali swala 5 hivyo wakati tunatoka
Polisi muda wa kwenda Msikiti ulifika.
Baada ya
kutoka Msikiti njini alikutana na Matapeli wanaofuatilia habari za harambee ya
ujenzi wa nyumba yake kwenye Mtandao wa Shekidele, Magazeti na Redio.
Matapeli hao
wakamsimamisha na kumueleza hivi.
“Tunaona
Shekidele anakupambani sana bosi wetu ameona habari zako hivyo ametutuma
tukutafute akuchangie mabati na Cement
sasa kama una lakini moja tupe tukodi gari sasa hivi twende na wewe ukavibebe
vitu vyako”
Matama
aliwaambia kwa muda huo alikuwa na elfu
50 tu Matapeli hao wakajifanya kumpigia simu bosi wao, baada ya kukata simu hiyo
ya uongo wakamueleza Matama kwamba bosi wao ametuma elfu 50 hivyo awape hiyo 50
waende kwa wakala wakatoe wakodi gari wampitie waende kuchukua vifaa hivyo.
Matama amezama msukoni na kuwakabidhi pesa, wajomba
wamelala mbele wakimuacha matama akiendelea kusubiri kwa zaidi ya masaa 2 bila
mafaniko.
Ndipo
alipoamua kumpigia simu Shekidele huku akiangua kilio Mwanahabri huyo alipofika awari alibeba jukumu la kumbembeleza na
kumueleza maeneo ya faraja aliokaa sawa
nikamruhusu erejee nyumbani tuonane kesho.