Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, March 23, 2026

WASIFU MZITO WA MWENYEKITI WA MTAA HAYATI HASSAN MSUNGI.


Hayati Hasan Msungi mwenye suti aliyesimama enzi za Uhai wake.



  Ally Msungi akizungumza na Mtandao huu juzi.


           Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

MPENDWA Msomaji wa Mtandao Pendwa wa Shekidele, jana tuli ripoti habari ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Saadan Kata ya Mwembesongo Mkoani hapa,Hassan Hussein Msungi[46].aliyefariki wiki niliyopita kwenye ajali iliyotoka maeneo ya Nane Nane.

Katika habari hiyo tuliahidi leo kurusha Wasifi Mkubwa wa hayati Msungi,aliyekuwa kipenzi cha Wana Mwembesongo na Morogoro kwa ujumla.

            WASIFU WAKE  HUU HAPA.

Akihojiwa na Mtandao huu msemaji wa familia Ally Msungu alitoa wasifu wa kaka yake kama ivuatavyo.

Hayati Msungi alizawali Mwaka 1980 Mtaa wa Saadani kata ya Mwembesongo,alisoma Shule ya Msingi Mwembesongo, na baadae akaenda  kusoma shule ya dini Mkoa lringa  inayojulikana kwa jina la Dur- Dabal.

Msema huyo ameendelea kusema, baada ya kumaliza elimu hiyo alirejea Morogoro na moja kwa moja alichaguliwa kuwa kiongozi wa dini ya Kiislamu mkoani Morogoro katika ofisi za Al-Masid akiwa msemaji wa Taasisi hiyo.

Kama hiyo haitoshi hayati Msungi alikuwa Mwanaharakati wa Umoja wa Vijana wa Kiislamu katika taasisi ya Tanzania,akijihusisha na kutoa Misaada  katika Vituo vya watoto yatima Tanzania.

          NDANI YA UWANJA WA SIASA.

Hayati Msungu aliyeacha Mjane mmoja na watoto watano alikuwa Kiongozi wa chama cha Wananchi CUF akishika nafasi ya Ukurugenzi wa Mipango na Uenezi wa Chama hicho Wilaya ya Morogoroo.

Aidha hayati Msungi alifanikiwa kikubwa Chama Cha Mapinduzi[CCM] nakufanikiwa kushinda uchaguzi Mkuu wa serikali ya Mtaa wa Saadan kwa Vipindi viwili mfurulizo  Mwaka. 2009 na 20014.

Uchaguzi wa Mwaka 20019 Hayati Msungi alibwagwa na Mdogo wake Ally Msungu anayeongoza mtaa huo mpaka sasa.

Ally MsungI aliyeshinda kwa leseni ya CCM alisimulia A-Z alivyopambana na kaka yake na kufanikiwa kumshinda, huku ndugu Mwingine wa Familia ya Msungi akiingilia kati akipinga maelezo ya Ally kwenye usnidi huo.

Utamu wa habari hiyo utaruka hivi punde hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao Pendwa wa Shekidele muda wote.

                           


No comments:

Post a Comment

MAJAJI 2 WAHUDHURIA IBADA YA KUMUOMBEA KIGOGO WA SUA MAREHEMU DKT MBILU.

         Mchungaji Dkt Rhoda Chamshama akiongoza ibada hiyo Katibu Mkuu wa  KKKT Usharika wa Mji Mpya Mshana akimuaga Mzee wake wa kanisa S...