Matama na
mkewe wakizungumza na Mwandishi wa habari.
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KABLA ya kutaja wema aliofanya aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Saadan Hayati Hassan Msungi kwa Ndugu yetu Mohamed Matama ambaye ni Mlemavu wa Miguu, nieleze kwa ufupi sababu za Mwenyekiti huyo kuguswa na kutoa msaada huo.
Matama anayeishi Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesongo jirani kabisa na Mtaa wa Saadan anaendesha Maisha yake kwa biashara ya kuuza Maji Mitaani na kwenye viwanja wa Mpira akitumia usafiri wa baiskeli.
Takribani Miezi miwili Mwandishi wa habari hizi hajamuona Matama Mtaani wala kwenye viwanja wa Mpira jambo ambalo si kawaida yake.
Hali hiyo ilimsukuma Mwandishi huyo kwenda nyumbani kwake kumjulia hali na kujua kipi kinamsibu.
Alipofika alimkuata Matama amejikunyata na Mkewe Bi Maua Said na alipoulizwa kulikoni haonekani alijibu.
“ Shekidele kwanza ubarikiwe sana kwa moyo wako wa huruma,kilichonifanya sionekani mtaani kwa muda mrefu ni Vibaka[ Mateja] wameiba miguu yangu kama unavyojua baiskeri yangu haingia ndani mlango ni mdogo miaka yote inalala hapo Nje.
Sasa Mwezi uliopita Mateja hao wamekuja na Misumeno wameikata kata na kwenda kuuza vyuma chakavu kulipokucha mimi na mke wangu tumeshuhudia mabaki ya vyuma ilituumiza sana kwa sasa mimi na mpendwa mke wangu hatuna uwezo wa kupata laki moja na Nusu kununua baiskeri nyingine ndio maana umeona sielewi nipo tu nyumbani” alisema Matama kwa sauti ya kinyonge.
Alipoulizwa kwa sasa anapataje pesa ya matumizi?
Alijibu.” Kukicha mke wangu anakwenda kufanya kazi ya kufua kwenye majumba ya watu akilipwa elfu 4 au 5 tunanunua chakua maisha yanaenda”
Kuptia Mwandishi wa habari hivi Mungu amefanya jambo Matama amepata baiskeri mpya kama hiyo haitoshi amenunua kiwanja na kujenga nyumba kubwa ya kisasa, nini kimetokea endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.



No comments:
Post a Comment