Dkt Aziz Abood akizungumza na wajasiliamali wa Jimbo la Morogoro
Leones Mvungu akifunga mkutano huo
Na Dustan shekidele Morogoro.
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro MjIni kwa Leseni ya Chama cha Mapinduzi [CCM] Mhe Abdulaziz Mohamed Abood Almaarufu Aziz Abood,ameapa kupambana na baadhi ya watumishi wa serikali wanaotumia vibaya pesa za mikopo ya vikundi vya wajasiliamali zinazotolewa na serikali kuu ndani ya Jimbo lake.
Mhe Abood ametoa kauli hiyo ljumaa iliyopita ndani ya ukumbi wa Tanzanite uliopo eneo la Msamvu Mataa.alipokutana na Vikundi vya Wajasiliamali kutoka kata zote 29 za Jimbo la Morogoro Mjini.
“ Kabla ya kukutana na nyinyi hii leo nimefuatilia na kubaini kwamba pesa za mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali nyingi haziwafikii walenga.
Pale ofisni utakuta mtumishi wa serikali anatengeneza kundi cha familia yake wanajikopesa hizo pesa” amesema mhe Abood na kukatishwa na shwange kubwa akishangiliwa na wajasiliamalia hao ambao wengi wao ni wanawake.
Baada ya shangwe hizo zilizodumu kwa takribani dakika 1 kunyamaza Mhe Dkt.Abood aliyeonyesha wazi wazi kukerwa na jambo hilo aliendelea kufunguka.
“ Nahidi tarehe 29 mkinichangua tena kwa kushirikiana na viongozi wangu wa chama yuko hapa katibu Mkuu nitashirikiana nao kupambana na watumishi hao na kuhakikisha wahusika ambao ndio nyinyi mnapata mikopo hiyo tena kwa wakati kwa sababu hilo lipo ndani ya ilani ya chama ” alimalizia kusema Mbunge huyo na kupokea zawadi ya lundo la Vigeregere na makofi ya kutosha.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Vikundi vya wajasiliamali hao Bw Leonis Mvungu akifunga mkutano huo alisema.
”Mhe Mbunge sisi wajasiliamali tunakupenda sana tazama juzi tu yaani siku mbili zilizopita ndio uliomba kukutana na hawa wajasiliamali kwa siku hizo chache umekuja umati huu mkubwa wengine wamejaa huko nje baada ya kukosa nafasi.
Naamini ungetuambia mapema wangekuja zaidi ya hawa”alisema Mvungu.
Akizungumza na Mtandao huu baada ya kutamatika kwa mkutano huo Mvungu alisema
”Mimi ninavikundi 390 na kila kukundi kina watu zaidi ya 20 shekidele wewe ni shahidi hupo kwenye moja ya vikundi vyangu sina ubabaishaji kwenye shughuri hii”alisema Mvungu.
Mkutano huu umehudhuriwa na Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Morogoro Bw Nuru John Ngereja.Katibu wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Bw Twalib Berege na Katibu Hamasa,Uenezi na Uwezeshaji Bw Maulid Chambilila.
Mhe Abood ambaye pia ni Mfanyabiashara Maarufu Tanzania akimiliki Mabasi,Malori, Viwanda, Vyombo vya habari na Vituo vya Mafuta[Sheli] amechaguliwa kwa kishindo kwenye kura za maoni ndani ya chama chake cha CCM.
Kufuatia kuridhishwa na utendaji kazi wa Mbunge huyo wanachama wa CCM Jimbo la Morogoro Mjini kwa kauri moja wamempitisha kugombea tena kwa mara ya 4 mfurulizo, Mhe Abood aliingia Mjengoni Dodoma kwa mara ya kwanza 2010.
ABOOD APA KUPAMBANA NA WANAOCHAKACHUA PESA ZA WAJASILIAMALI.