Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, August 11, 2025

KUMBUKIZI WAZEE MASTAA WA JIJI A MWANZA


 

Mmiliki wa Mtandao huu Dustan Shekidele[kushoto] akiwa na Wazee Mastaa wa jiji la Mwanza.

 

Wazee hao mbali na ustaa wao pia watoto zao kwa nyakati tofauti wametamba na timu kubwa za Simba na Yanga.

 

Wazee hao si wengine ni Mzee John Tegete[pichani] nyuma ya pikipiki ya ‘Ez Come Ez Go’ nikimtembeza mitaa mbali mbali ya Mji Kasoro bahari nazungumzia Morogoro.

 

Picha no mbili  Mzee Alfan Ngaza pichani kulia akizungumza na Shekidele ndani ya uwanja wa Jamhuri Morogoro, wazee wote hawa waifika mkoani Morogoro kwa nyakati tofauti wakiwa makcha wakuu wa timu ya Toto Afrika ya Mwanza wakati huo ikiwa Ligi daraja la kwanza.

 

Ifahamike Mzee Tegete pia ni Meneja wa Uwanja wa CCM Kirumba wa Jijini Mwanza

Kama hiyo haitoshi Mzee Tegete Mwanae Jerryson John Tegete amewahi kuwinga na timu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania.Taifa Stars’

 

Huku Mzee Ngaza Mwanae Mrisho Alfan Ngassa amewahi kuwika na timu za Yanga, Simba na Azam pamoja na timu ya taifa ya Tanzania.

 

Mtoto mwingine wa Mzee Ngassa  Beno Ngassa kwa sasa anatamba na timu ya Tanzania Prisons  akiwa mshambuliaji tegemeo wa wajela jela hao wa Jijini Mbeya.

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...