Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, April 11, 2025

SIMBA KUTINGA NUSU FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO MLEMAVU AMTOA MACHOZI SHABIKI WA YANGA








 

.

      Na Dustan Shekidele,Morogoro.

 UKISTAAJABU ya Mussa hutoyaona Filahuni.

  Baada ya Simba kutinga Nusu fainali michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika,Shabiki lia lia wa Simba Matheo Msagati Maarufu ‘Matheo wa Kilosa’ambaye ni Mlemavu  wa Miguu amemtoa machozi Shabiki Kindaki ndaki wa Yanga Shabani Salim Maarufu Shabani Yanga.

 Tukio hilo la kushangaza lililojaza umati mkubwa wawatu limetokea Leo majira ya saa 10 jioni Mtaa wa Makongoro uliopo katikati ya Mji wa Morogoro kwenye  ofisi ya kubani nyimbo inayomilikiwa na shabiki huyo wa Yanga.

    KISA NA MKASA WA TUKIO HILO HUU HAPA.

Kama kawaida mara baada ya kutokea kwa mtiti huo uliofunga mtaa baadhi ya raia wema fasta walimtwangia simu Mwandishi wa habari hizi mwenye rasilimali kubwa ya watu ’sos’waliosambaa mitaa mbali mbali ya Mji wa Morogoro walimtwangia simu na kumrambisha ubuyu huyo.

Fasta Mwanahabari huyo alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendo kasi ‘Boxer Ez Come Ez Go’na kufika eneo la tukio ndani ya dakika o  na kushuhudia songombingo hiyo likiwa limepamba Mto kama ule wa Kifuu.

Moja kwa Moja Paparazzi huyo aliegesha chombo yake kando ya barabara na kupangua msitu wawatu na kuwafikia mashabiki hao  ambapo walipo hojiwa walikuwa na haya ya kusema.

 WAKWANZA KUFUNGUKA NI SHABIKI WA SIMBA

“ Baada ya timu yangu ya Simba kufungwa bao 2-0 kule Misri huyu mtani wangu aliniambia Simba ameshatolewa haina uwezo wa kumfunga Mwarabu Dar na kutinga Nusu fainali.

Nikamwambia kwa mpira mkubwa tulioupiga kule Misri Kwa Mkapa Mwarabu namfunga hata kabla ya misa ya kwanza kuanza tukabishana sana kia mtu akishikilia msimamo wake” alisema Matheo wa Kilosa na kuendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi.

Mwisho wa ubishi Shabani kaniambia tuweke bima mbele ya ushahidi tukawewa bima kwa vile mimi sina mali zaidi ya baiskeri yangu tukakubalia kwamba Simba asipotinga Nusu fainali achukue hii baskeri yangu na yeye kasema simba akingika Nusu fainali nije kubeba hii ofisi yake yote ya kubani nyimbo.

Simba katinga Nusu fainali nimekuja hapa na usaifi kubena ofisi hii chaajabu wakati tunakusanya vitu Jamaa anaangua kilio kama mtoto akidai kwamba ameadhiriki watoto zake watakufa njaa kwa sababu anategea ofisi hii kuendesha maisha ya famiia yake.

Baada ya kuangua kilio na kuwataja watoto zake kufa njaa kama binadamu nimeguswa na hao malaika wa Mwenyezi Mungu nimeamua kumsahe na kumuachia ofisi yake kwa sharti kwa siku nyingine asiudie tena kuiweke bima Simba vinginevyo  nitamfanyia ubaya ubwela”alisema Matheo wa Kilosa.

 Kwa upande wake Shabani Yanga huku akimwaga machozi alisema.” Ni kweli tuliweka Bima na huyu Matheo wa kilosa kinachoniliza angechukua ofisi hii ningeishije wakati ninamke na watoto nategemea ofisi hii,kipekee namshukuru sana kwa kunisamehe ndio maana umeona kwa furaja nimejikuta namwafa machzi na kumkumbatia  sikuamini kama amenisamehe toka juzi simba alivyofuzu  siku lala nilikuwa Nawaza ofisi yangu kuondoka, hivyo leo naona nitalala vizuri na sitoludia tena kufanya mchezo kama huu”alisema Shabani  na kuendelea kumwaga machozi ambapo Mwandishi wa habari aliamua kubeba jukumu la kumbembeleza huku Matheo akipiga pedeli baiskeli yake na kuondoka zake.

Mnyama Simba mwenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi Kariakoo jijini Dar juzi Jumatano alifanikiwa kutinga Nusu fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika[CAF] baada ya kuitoa timu ya Al-Masry ya  Misiri kwenye mchezo wa Robo fainali na kufanikiwa kutinga Nusu fainali kwa mara ya pili huku akifanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1993.

No comments:

Post a Comment

KIJIWE NONGWA. UKIONA KAFUTA BANGO UJUMBE UMEFIKA

  Na Mpekunyuzi wa Mitandao Dunstan Shekidele.   Kama kawaida mtumishi wako, kila wiki naweka Bando linalonitembeza kwenye Mitandao ya Kijam...