Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, November 4, 2024

MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU.MADENT 4 WENYE MATATIZO YA AKILI WAMEFAULU MTIHANI WA DARASA LA SABA.



Denti wa darasa la pili shule ya Msingi Nane nane Gidion Samwel[11]mwenye ulemavu wa viungo akiwa na mama yake mzazi Bi Eulester Ally.

 

Mwalimu Sarah   akizungumza na Mwandishi wa habari hizi huku akimuonyesha mmoja wamadent wenye ulemavu, pembeni yake aliyevaa shati jeusi ni Mwenyekiti wa shule hiyo Mzee Taiko..

 

 

 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

UKISTAAJABU ya Mussa Hutoyaona ya filauni. Wanafunzi wanne wenye matatizo ya Mtindio wa Ubongo wamefaulu mtihani wa darasa la saba huku baadhi ya madeni wenye akili timamu wakiferi mitihani hiyo.

Kama kawaida kila wiki Mwandishi wa Mtandao huu huzunguka mitaani kusaka habari  moto moto  na kuzirusha hewani kila jumatatu kwenye mtando Pendwa wa Shekidele.

Sote tunafahamu wiki iliyopita matokeo ya taifa ya Darasa la Saba yalitoka hadharani na wazazi wengi walizunguka kwenye mashule kuangalia matokeo hayo.

Kufuatia hali hiyo Mwandishi wa habari hizi alijiongeza akatinga shule ya Msingi Nane nane ambayo inadarasa maalumu la wanafunzi wenye matatizo mbali mbali ya ulemavu.

 Mwanahabari huyo alipofika kwenye shule hiyo alishuhudia baadhi ya wananchi wakishikwa na butwaa baada ya kushuhudia wanafunzi 4 wenye ulemavu wa Utingio wa Ugongo wakifaulu mtihani huo .

 “ Acheni Mungu aitwe Mungu tumefika hapa kuangalia matokeo wa darasa la Saba tumeshuhudia wanafunzi wenye matatizo ya akili wakifaulu kwenda sekondari huku baadhi ya wanafunzi wenye akili timamu wakiferi ”alisema mmoja wawananchi alijiyetambulisha kwa jina la Asha Bakari.

Ili kupata uthibitisho na ufafanuzi wa jambo hilo Mwandishi wa habari hizi alimtafuta Mwalimu wa Shule hiyo Sarah Sima ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha watoto wenye ulemavu ndani ya shule hiyo.

“ Ni kwelie tunamshukuru Mungu wanafunzi wanne wenye matatizo ya akili wamefaulu mtihani wa darasa la saba kwa sasa kama ilivyo kwa wanafunzi wengine nao wanasubiri kupangiwa shule ili wakaanze kidato cha kwanza”alisema Mwalimu Sarah.

Alipotakiwa kuwataja wanafunzi  waliofaulu Mwalimu huyo huku akiwa na furaha alisema

“ Wanafunzi hao ni Ally Mmasi. Martin Francis.Alafa Mboma na Braiton Mapunda.”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shule ya Msingi Nana nane Gogfrey Taiko alipohojiwa  alisema shule hiyo imeanzishwa Mwaka 2002 ikiwa na darasa hilo la watoto wenye changamoto mbali mbali za ulemavu.

”Hawa watoto wenye ulemavu nao wanahaki ya kupata Elimu tunaishukuru serikali  kuanzisha vitengo hivi vya Elimu kwa wanafunzi wenye ulemavu ona sasa wanafunzi wetu 4 wa shule yetu wamefaulu kwenda sekondari”alisema Taiko ambaye ni Polisi Mstaafu.  

                        


No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...