Kocha Hussein Mau
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
KAMA Kawaida mtandao pendwa wa Shekidele wiki nzima unasaka habari moja kubwa iliyochukua nafasi kwenye mitaa na kuiongezea ‘nyama’ kwa kuzungumza na wadau wanaohusika na habari hiyo kwa lengo la kupata ufafanuzi zaidi.
Wiki iliyopita Fagia la Mtaa lililobebwa na Mwandishi wa Mtandao huu lilizunguka mitaa mbali mbali ya Mji Kasoro bahari ‘Morogoro’ likifagia mitaa kwa lengo la kusaka habari kubwa ya wiki.
Fagia fagia hiyo ilishuhudia Wanamorogoro wakilalamika kitendo cha mchezaji wao kutoka Milima ya Kinole Morogoro Kibwana Shomari kuwekwa benchi na nafasi yake kucheza Denis Nkane ambaye ni mshambuliaji anayetokea winga ya kulia.
“Mimi ni shabiki wa Simba kwenye hili niwe mkweli,baada ya Yanga kumsajiri Yao Yao Kwassi kibwana Shomari kukaa benchi niliafiki Kwa sababu Kwassi anauwezo mkubwa kuliko Kibwana.
Baada ya kwassi kaumi nilitegemea Mluguru mwenzangu Sekulu Kibwana angepata nafasi ya kucheza, kwa mshangao wawengi Kocha wa Yanga kaendelea kumuweka Kibwana benchi kamtoa Nkane Mbele aje kucheza nafasi ya Kibwana hii kwangu sio sawa” alisema Joseph Msimbe.
Kufuatia malalamiko ya wadau hao wa soka mkoa wa Morogoro Mwandishi wa habari hizi aliwatafuta Makocha wa Moro Kids Hassani Mnyani ‘Maarufu Ticha Majuto’aliyekuwa akiifundishi timu ya Moro kids ya watoto wenye umri wa kuanzia miaka 7 mpaka 16 na Hussein Mau[Mwenye kofia kichwani] aliyekuwa akiifundisha timu ya Moro Kids ya watoto wa miaka 16 mpaka 20.
Vijana hao wanapofika miaka 20 Moro Kids huwapeleka timu za Mtibwa B, Azam B. JKT Tanzania na timu mbali mbali za Ligi daraja la Kwanza na la Pili.
Mahojiano yetu na makocha hao yalikuwa hivi.
Mwandishi. Habari zetu walimu.
Ticha Mau. Njema karibu Shekidele kwenye duka letu la Vifaa vya michezo.
Mwandishi . Asante najua wachezaji wengi wanaong’ara Ligi kuu kwa sasa wamepitia kwenye mikono yenu kwa faida ya msomaji wa Mtandao wa Shekidele tutajie baadhi ya wacheaji hao.
Ticha Mau. Wako wengi sana baadhi yao ni Dickson Job, Kibwana Shomari. Nickson Kibabage.na Abuutwalib Msheri. [Yanga]
Shomari Kapombe, Mzamiru Yassini na Ladack Chasambi[Simba]
Pascal Msindo [Azam]
Shiza Kichuya[JKT Tanzania]
Offen Chikolla[Tabora United]
Hamad Waziri’Kuku’ Singida Big Stars
Na Masenga Tanzania Prisons.
Mwandishi. Kwa sasa wadau wengi wa soka hasa morogoro wanalalamikoa Kibwana shomari kukaa benchi na nafasi yake kuchezeshwa mchezaji wa mbele nyinyi kama makocha mlioibuka kipaji cha mchezaji huyo mnalipi la kusema ?
Ticha Mau. Hata sisi jambo hilo linatushangaza kiukweli Yao Yao Kwassi ni mzuri zaidi ya Kibwana alipoumia kwassi tulitarajia
Kibwana angecheza kwasababu ndiye mbadala wa Kwassi.
Hivyo Kitendo cha kocha kuendelea kumuweka benchi huku nafasi yake akicheza Nkane landa kuna tatizo la utovu wa nidhamu kwa mchezaji lakini kiukweli kibwana bado ni mdogo na taifa
linamtegemea kwenye timu ya Taifa kitendo cha kocha kumuweka benchi ni kuua kipaji chake.
Mwandishi. Kwa maelezo hayo Je ukipewa nafasi ya kumshauri utamshauri nini Kibwana Shomari?
Ticha Mau. Nitamshauri atafute malisho sehemu nyingingine kulinda kipaji chake.
Mwandishi. Asante ticha Mau.
Kwa upande wake Ticha Majuto alipotakiwa kuelezea lile Pato la Kibabage na Chikola kwenye gemu ya Yanga na Tabora alisema.
“Shekidele bado lile lilinifurahisha sana wanangu kisoka Kibabage na Chikolla walionyeshana ufundi ndio maana leo nimevaa hii jezi ya Chikolla aliniletea wakati akiwa Geita Gold nyuma ina jina lake soma uone”alisema ticha Majuto na kuendelea kudadavua.
“ S Leo nimevaa ya Chikolla Kesho navaa jezi aliyoniletea Kibabage, wakati wakiwa na umri wa miaka 15 kwenye timu yangu Chikolla alikuwa akicheza nyuma na Kibabage mbele.
Kwa sasa Kibabege anacheza beki ya kushoto na Chikolla anacheza winga ya kulia juzi wamekutana na kuonyeshana umwamba Chikolla kaibuka mbeba kwa kupachika bao 2 mbele ya Kibabage”alimalizia kusema ticha Juto.
Clips Video ya mahojiano na makocha hao itaruka hewani hivi punde mitandao ya Shekidele ya lnstagram na Facebook
No comments:
Post a Comment