Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, August 27, 2024

PIchani hii inayoonyesha Mji wa Morogoro niliipiga nikiwa juu ya Kilele cha Milima ya Uluguru.
Mwandishi wa Mtandao huu akionyeshwa moja ya mashamba yaliyopo juu ya Mlima huo na Mmiliki wa shamba hilo [hayupo pichani].
.......Nikitua Juu ya Kilele cha Milima ya Uluguru na Boda boda yangu ambayo iliniwezesha kufika kwenye kilele hicho

 Baada ya kushuka niliamu kupiga picha Mlima huom kumbuka nilikuwa juu kabisa ya Kilele cha Mlima huo wa Uluguru

UTALII WA NDANI.

Kuna nyakati Watanzania tunapaswa kutalii kwenye vivuti vyetu, pichani Mwandishi wa Mtandao huu aliamua kupanda juu ya kilele cha Milima ya Uluguru kwa kutumia boda boda yake.

Juu ya Milima hivyo kuna vivutia vingi miongoni mwao ni Ndege na Vyura ambao dunia nzima wanapatikana kwenye mlima huo pekee.

Kivutia kingine ni eneo la ‘Morning Site’ eneo hilo siku zote linaonekana ni asubuni likitandwa na mawingu na kwamba hata jua liwake vipi halifika eneo hilo January Mpaka Desemba.

 Kwa maajabu ya Mwenyezi Mungu Muumba wa Mbingu na nchi muonekana wa eneo hilo ni kama  limeezekwa kitu cha Kuzuia Mwanga juu yake lakini ukiangalia juu hakuna kitu chochote.

Najiandaa kupanda tena juu ya Mlima huo kwa lengo la kupiga picha vivutia hivyo na kuvitanga kwa lengo la kuwavutia watalii na kuingiza mapato Mkoa wetu wa Morogoro.

Juu ya Milima hiyo nimeshuhudia watu wakilima mazao mbali mbali kando kando ya Mito iliyozaliwa na miti ya Milima hiyo.

Wakati nashuka juu ya Milima hiyo nilisimamisha pikipiki na Kupiga picha Mji wa Morogoro, picha hiyo unaweza kuzani imepigwa na kamera ya Juu ’Drone’ kumbe nimeipiga na kamera yangu ya kawaida nikiwa juu ya Milima hiyo.

Hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu kushuhudia vivutia hivyo kama nitafanikiwa kupata picha za Ndege na Vyura hao pamoja na eneo la Morning Site

Nikiwa huko huko juu nyakati za jioni nilishuhida Mwezi ukichomoka nyuma ya Milima hiyo jambo ambalo pia lilinishangaza.

[Picha zote na Dunstan Shekidele Morogoro.]

 

 

Drone Camera.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...