Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, August 21, 2024

KUMBUKIZI MSANII DIAMOND PLATNUMZ ENZI HIZO.





 


Mwandishi wa habari Dunstan Shekidele ’Mkude Simba’ anaweza kuwa sehemu ya Mafanikio ya Msanii nyota Afrika wa Muziki wa Kizazi Kipya ‘Mwamba’ Nassib Abdul Maarufu Diamond Platnumz Baba Tiffa.

Kwa sehemu kubwa Mwanahabari huyo aliandika habari nyingi za Diamond kwenye Magazeti Pendwa ya Global Publishers tunazohisi zilimuongezea umaarufu.

Pichani Shekidele akimhoji Diamond kwenye Tamasha la Vodacom lililofanyika takribani miaka 10 iliyopita kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro na kuhudhuriwa na Umati mkubwa wawatu kwa kiingilio cha Free Mandela ‘Bure’

Picha hizo kali za Diamond zilizopigwa na Shekidele zilitumika kwenye  Magazeti ya Global na Mitandao ya Kijamii ya kampuni hiyo.

Kwa sasa Diamond Mzaliwa wa Kigoma ni Miongoni mwa wasanii matajiri barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

VITUKO VYA MWEZI JANUARI

  Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya.   Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...