Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, June 19, 2024

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHO MWA WIKI. BAND ZA WALUGURU OG NA MAISHA MAPYA KAMA SIMBA NA YANGA






 

.

Na Mlala Nje Dustan Shekidele,Morogoro. 

BAND mbili Maarufu za Muziki wa dansi mkoani Morogoro, Waluguru Original na Maisha Mapya wameingia kwenye vita kali ya kunyang’anyana wanamusiki, kama ile vita ya Simba na Yanga ya kugombea wachezaji.

Takribani Miezi mitatu iliyopita Mlala Nje alitinga kwenye shoo ya Waluguru Og na kumshuhudia Mwimbaji nyota wa band ya Maisha Mapya Juliana Mgella akitambulishwa kujiunga na band hiyo inayomilikiwa na Mluguru Deogratius Aluphonce ‘Maarufu Killer Boy’.

Hivi karibuni Mlala nje alitinga kwenye shoo ya Band ya Maisha Mapya na kushuhudia band hiyo inayomilikiwa na Mkaguru Joshua Malekea ‘Maarufu Joshkera’wakijibu mapigo kwa band ya Waluguru Og kwa kumnyakua  Amina Remmy Maarufu Emmy wa Remmy.

Wachambuzi wa mambo wamedai kwenye vita hiyo band ya Maisha Mapya ndio walioramba dume kwa kumnyakua Emmy ambaye anapiga miguu yote miwili nikiwa na maana kwamba anaimba na kucheza tofauti na July  anayepiga mguu mmoja tu wa kuimba. 

Pichani Emmy akitambulishwa na band ya Maisha Mapya ambapo wakati akitambushwa alipanda jukwaani kwa Style ya kunesanesa huku akinengua, baadae  alikamata Mic na kuimba wimbo wa ‘Maproso’akikong’a nyoyo za mashabiki kwa sauti yake tamu tamu.

Wiki end ijayo Mlala nje atatinga kwenye shoo ya Waluguru Og kuona kama Big Boss Kille Boy ‘Mluguru Og’atajibu mapigo kwa mara nyingine kunyofoa Mwanamuziki wa band ya Maisha Mapya ‘ Full Vipaji.’

Kwenye vita hiyo ya Mluguru[Killer Boy pichani mwenye suti ya damu ya mzee] na Mkaguru Og[Joshua]pichani anayepiga gitaa wote kutoka Mkoa wa Morogoro.

 Joshua akitoka Kijiji cha Msingisi Jimbo la Gairo linaloongozwa na Mbunge Mhe Ahmed Shabiby ambaye ni mmiliki wa kampuni ya mabasi ya Shabiby Line na Killer Boy anayetoka Kijiji cha Mkuyuni Jimbo la Morogoro Kusini mashariki linaloongozwa na Mbunge Mhe Hamis Tale tale Maarufu Babu Tale ambaye pia ni Meneja wa Msanii Maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Afrika Nasbu Abdul ‘Diamond’

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...