Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, March 25, 2024

MAANDALIZI MAZURI NI KUTENDA MAMBO MEMA NA SI KUJIICHIMBIA KABURI NA KUJINUNULIA JENEZA.


  Hii ni Mfano wa kaburi na Jeneza alilojitengenezea Afande huyo Mstaafu.


             Na Dustan Shekidele,Morogoro.

NIMESUKUMWA na roho mtakatifu kuelezea jambo hili kwa taifa la watu wa Mungu walipo pande zote za dunia.

Hivi karibuni nilisikia na kusoma kwenye vyombo vya habari kwamba kuna Mtu hapa Tanzania amefanya maandalizi yake ya kifo kwa kujichimbia kaburi.

Kama hiyo haitoshi mtu huyo ambaye tunamuhifadhi jina juzikati ameendelea na maandalizi hayo kwa kujinunulia jeneza la thamani na kuitisha mkutano wa waandishi wa habari na kutangaza jambo hilo.

Kwangu mimi naona jambo hilo haliko sawa mbele za Macho ya Mungu kwa sababu kifo ni siri ya Mungu na Mwanadamu,sote hatujui tutakufa lini na tutakufa je.

Unaweza kufanya hayo yote kwa nia njema lakini kifo chako kikawa tofauti ukafa kwa kusombwa na mafuriko yakakutupa baharini ukamezwa na Mamba na mwili wako usionekana.

 Hivyo maandalizi hayo ya kujichimbia kaburi na kujitengenezea Jenera yatakuwa hayana maana kwa sababu mwili wako haukuonekana baada ya kumezwa na Mamba.

Mimi kwa akili yangu fupi nadhani maandalizi mazuri tukiwa hai ni kumcha Mwenyezi Mungu na kutenda mambo mema yatakayokupa tiketi ya kwenda peponi na si kujichimbia kaburi na kujinunulia Jeneza.

Namshauri kaka yangu huyo Afande ambaye kimsingi namfahamu vizuri na yeye pia ananifahamu vizuri kwani alifanya kazi nzuri ya Upolisi  

Askari polisi huyo awari alikuwa hapa Mkoani Morogoro kabla ya kuhamishiwa Mkoani Mara  na hivi karibuni kustaafu kazi na kurejea nyumbani kwao kwenye moja ya mkoa ulioo kaskani mwa Tanzania na kufanya maandalizi hayo ya kujichimbia kaburi na kujinunulia Jeneza.  


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...