Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, February 9, 2024

RAIS TFF ASHUHUDIA KIHANGA AKICHAGULIWA TENA KUWA MWENYEKITI CHAMA CHA SOKA MKOA WA MOROGORO’MRFA’

Mwenyekiti wa kati ya uchaguzi akitangaza matokeo jana
Mh Pascal Kihanga akitabasamu baada ya kutangawa kuwa Mwenyekiti wa chama cha Soka Mkoa wa Morogoro'MRFA
....Mh Kihanga akipongewa na wajumber pamoja na mgeni rasm
.                 Rajabu Kiwanga Mwenyekiti Mpya MRFA
CPA Peter Mrukwamba Mshighati Mtunza fedha Mkuu MRFA
               Hassam Mtemba Mjumbe kamati wa utendaji
            Charles Mwikola Mjumbe no 2 kamati ya Utendaji
Uchagu huo umejanyika jana kwenye jengo hili jipya la halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, lililopo  Mtaa wa Nunge zamani eneo hili palikuw ana jengo dogo la ukumbi wa DDC

 

  

          Na Dustan Shekidele   Morogoro.

 Licha ya maneno mengi ya ‘Nongwa’ya wadau wa soka nchini,juu ya Mwenyekiti wa chama cha soka Mkoa wa Morogoro, [MRFA] Pascal Kihanga, hayakufua dafu mbele ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa MRFA,ambapo Makamo wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania’TFF’ Athuman Amlani, ameshuhudia wajumbe hao wakimchagua kwa kishindo Kihanga kuongoza tena chama hicho kwa miaka mingine Nne.

Uchaguzi huo uliopooza umefanyika jana kwenye ukumbi Mpya wa Mbaraka Mwinshehe unaomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Katika hali ya kushangaza Mwandishi wa Mtandao huu hakuwaona ukumbini wajumbe wa Wilaya mbili za Kilosa na Morogoro Mjini inayoungana na Wilaya ya Morogoro Vijini kisoka.

Uchunguzi wa awari uliofanywa na Mwandishi wa habari hizi umebaini Wilaya hizo hazijafanya uchaguzi  hivyo kukosa sifa za kutuma wajumbe kwenye Uchaguzi huo.

 Wajumbe  12 Pekee ndio waliopiga kura badala ya wajumbe 20 wa Mkoa mzima,Wilaya zilizofanya uchaguzi kwa wakati na kutuma wajumbe kwenye mkutano huo ni Wilaya ya Kilombero,Gairo, Mvomero,Malinyi.na Ulanga.

 Mara baada ya mgeni rasm Kigogo wa TFF Athuman Amlani kufungua mkutano huo kisha kuzungumza machache akiwaagiza Viongozi watakaochagulia kuhakikisha wanainua soka la mkoani Morogoro.

Kwa mujibu wa katiba Mpya wa TFF wajumbe wa Mkuatno  Mkuu walipewa jukumu la kuchagua nafasi tatu za Mwenyekiti, Makamo Mwenyekiti na Wajumbe wawili wa Kamati tendaji.

Baada ya zoezi la kuhesabu kura kutamatika mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Wakili Michael Mwambanga alitangaza matokeo kama ufuatavyo.

Pascal Kihanga alichaguliwa tena nafasi ya Uwenyekiti.

Makamo Mwenyekiti alichaguliwa .Rajab Kiwanga kutoka lfakara Wilaya ya Kilombero.

 Huku Hassan Mtemba kutoka Gairo na Charles Mwikola kutoka Kilombero wakinyakua nafasi ya kamati tendaji.

           ZEGE HALILALI.

Kwa mamla aliyopewa na katiba Mpya ya uchaguzi TFF. Mara baada ya kutangaza mshindi Mwenyekiti Kihanga alimteua Jimmy Lengwe kuwa katibu Mkuu wa MRFA.

Nafasi ya mtunza Fedha Kihanga alimteua Peter Mvukwamba Mshighati.                  TUJIKUMBNUSHE.

Kihanga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mazimbu na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro anakiongoza chama hicho cha Soka kwa mara  ya tatu mfurulizo toka achaguliwe kwa mara ya kwanza kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka 2016.akichukua nafasi na hayati Mzee  Aman Komanya.

Kwenye nafasi yake hiyo ya uwenyekiti Mh Kihanga alifanyakazi na makatibu wakuu wengi akiwemo Charles Mwakambaya, Marehemnu Hamisi Semka, na Emmanuel Kimbawara aliyetimuliwa juzikati na nafasi yake ikashikwa  kwa muda na katibu mkuu Msaidizi Jimmy Lengwe aliyekura shavu jana la kuteuliwa kuwa katibu Mkuu.

Kwa pande wa Mhadhini Mshighati alichaguliwa kwa kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu wa MRFA Uliofanyika mwaka 2020 kwenye ukumbi wa Tax Palece akipata kura 34. Kwa uadilifu wake wa kutunza fedha za chama Mh Kihanga kwa mamlaka aliyopewa jana alimteua  tena Peter Mshighati kubaki  kwenye nafasi yake hiyo.

 Binafsi Mwandishi wa habari hizi anamfahamu vyema Mshighati amejawa na hovu ya Mungu ndio maana anakiongoza kitengo hicho cha fedha kwa welezi uliotukuka akimtanguliza Mungu mbele maslai yake binafsi akiyawake nyuma  kwa tabia yake hiyo vyema atafika mbali. 

           OMBI LA MTANDAO HUU.

Tunawaomba Viongozi waliochaguliwa na kuteuliwa  kuchapa kazi na kuhakikisha ndani ya miaka 2 Mkoa wa Morogoro unarejea kwenmye hali yake ya awari ya kuw ana timu nyingi kwenye madaraja yote.

 Inashangaza sana kuona wachezaji wengi kutoka mkoa wa Morogoro wanang’ara kwenye Ligi Kuu, Ligi daraja la Kwanza na Ligi daraja la Pili kwenye timu za Mikoa Mingine huku Mkoa wa Morogoro Viwanja vyake vya soka yanafanyika Mashindano ya Shimiwi, Shimuta Bandari,Matamasha ya Siasa. Dini na matamasha ya Burudani.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...