Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, February 15, 2024

PAMBA YA ZIDI KUCHANUA LIGI DARAJA KWANZA.

..Mshika kibendera namba 2 akinyoosha kuashirki mchezaji wa Transiti Camp ameotea
...Kocha wa Transit Camp akiwazuia wachezaji wake wasimvamie Refa
...Baada ya kushambuliwa mfurulizo kocha Mbwana Makata akitazama muda kila Mara akiomba mchezo utamatike
..Makata akiwapongeza marefa kwa kumaliza mchezo salama



Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TIMU ya Pamba Jiji ya Jijini Mwanza imezidi kuchanua ligi daraja la kwanza baada ya kuwachapa wenyeji wao Maafande wa Transit Camp bao 1-0.

Gemu hiyo ya ‘Champion Ship’ imepigwa jana Uwanja wa Jamhuri Morogoro unaotumiwa kama uwanja wa nyumbani na wanajeshi hao wa Transit Camp ya Jijini Dar es salaam.

Bao hilo pekee la ‘’Wana TP Lindanda’Pamba ‘Nyepesi’ Vijana wa Mkuu wa Mkoa Amos Makalla lilipachikwa wavumi dakika 9 baada ya Kiungo ‘fundi’ Daniel Jastin Jolam kupiga faulo nje ya 18

iliyokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha Kipa wa ‘wajeda’ hao Erick Mailo akiluka bila mafanikio.

Huku Mailo akipongezwa na wenzie kwa kufunga bao hilo safi ambalo kimsingi halina ‘umbewa’ wa kwenda kuchungulia ‘kulihakiki’kwenye ‘VAR’. Dakika 26 winga wa Transit Kalegea Wazanga aliambaa na mpira winga ya kushoto kamaliza uwanja kipa wa Pamba John Chacha alivyomfuata kamchambua kama Karanga na kumpa Pasi ya Upendo Saluma Ramadhan aliyebaki yeye na gori,wakati akijiandaa kufunga mshika kibendera namba 2 alinyoosha kipendera chake akidai Ramadhan aliyevalia jezi no 3 alikuwa eneo la kuotea.

Kama hiyo haitoshi dakika 89 Wajeda hao nusura wasawazishe bao hilo kama sio Vigisu Vigisu za refa kuuma ‘Muvu’ ya bao. 

 
lshu ilikuwa hivi Mshambuliaji wa Transit Camp Salum Ramadhan alifanikiwa kuwatoka mabeki wa Pamba, wakati akijianda kufunga, mchezaji mmoja wa Pamba aliyekuwa jirani na refa alijiangusha na refa kupuliza filipi ya kusimamisha mchezo jambo lililopelekea mashabiki wachache waliokuwepo uwanjani hapo kuamsha kelele za kumzomea refa huyo.

Kufuatia hali hilo kundi la wachezaji wa Transit Camp walimvamia refa wakitaka kumpiga hata hivyo kocha wa Maafande hao aliingia uwanjani na kuwatuliza wachezaji wake ambao walitii amri ya kocha wao na kumuacha refa huyo.

Dakika 4 za nyongeza Pamba walikata moto na kusababisha kushambuliwa hali iliyopelekea kocha Mkuu wa timu hiyo Mbwana Makata kushikilia roho muda wote akiangalia saa yake akiomba mpira uishe.

Huku mchezaji mpya wa timu hiyo Harun Chanongo aliyewahi kuitumikia Mtibwa Sugar mara baada ya gemu hiyoi kutamatikja alisikika akisema’ hawa Trans Kama siku zote wangecheza hivi kwa kujituma wangeongoza Ligi wanatukamia sisi tu”

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...