...Waumini hawa baada ya kuona mwaka Mpya walinyongea madhebahuni mwa Bwana na kuangusha maombi mazito ya kumshukuru Mungu kwa kuwafusha Mwaka mwingine
...Mchungaji Dunia akipongezana na waumini wake baada ya kufanikiwa kuona Mwaka Mpya
Waumini wakikumbatiana huku wakilia baada ya kufanikiwa kuona Mwaka Mpya wa 2024 juzi
Mwana kwaya akiimba sambamba na Mchumbaji
Mwinjilisti Nyange akiombea makundi mbali mbali.
Ibada zote za usharika huo zinaruka Live YouTube, mwaka Mpya ulipoingia Mtaalamu wa kurusha Live lbada hiyo Komred Kulwa aliweka kando Lap Top na kuingia kwenye maombi Mazito akimshukuru Mungu kwa kumpa kibari cha kuuona Mwaka 2024.
Kwaya ya kusifu na kuabudu'Kwaya ya Umoja' ikiimba kwenye mkesha huo juzi usiku
Mwanjilisti Godfrey Nyange akimtolea Mungu Sadaka
Na Dustan Shekidele,Morogoro.
WAUMINI wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania’KKKT’ Usharika wa Mji Mpya Jimbo la Morogoro, juzi Desemba 31 walikesha kanisani wakiuaga Mwaka 2023 na kupokea Mwaka Mpya wa 2024 kwa Vilio na Vicheko.
lbada hiyo ya mkesha ilianza saa 3 usiku na kutamatika saa 7 usiku, Mwandishi wa Mtandao huu aliyeshiriki mkesha huo alishuhudia mambo haya.
llipofika saa 6 kamili usiku kengere ya kanisa hilo iligongwa kiashirio cha kuingia kwa Mwaka Mpya 2024.
Baada ya kuingia kwa Mwaka Mpya na kuuga mwaka 2023, baadhi ya waumini wa kanisani hili waligawanyika wengine walinyongea Madhabahuni mwa bwana wakapiga magoti na kuangusha maombi mazito ya kumshukuru Mungu maombi hayo yaliambatana na vilio, huku kundi la Pili likikumbatiana na kuangua Vilio wakati wakiupokea Mwaka Mpya.
Kundi la tatu lilibaki kwenye viti na kuangua vicheko vya furaha huku waki luka luka kwa kufanikiwa kuona Mwaka Mpya.
Kabla ya kuingia Mwaka Mpya Mchungaji Kiongozi wa Usharika huo Mch. Sifu Thomas Dunia kwa kushirikiana na Mwinjilisti Godfrey Nyange kwa nyakati tofauti walialika makundi mbali mbali kunyongea Madhebahuni mwa bwana na kufanyiwa maombi maalumu.
Miongoni mwa Makundi hayo ni Kundi la Watu wasio na ndoa walifanyiwa maombi maalumu ya kupata ndoa Mwaka 2024, kundi lingine ni kundi la wanafunzi waliofanyiwa maombi maalumu ya kufanya vizuri kwenye masomo yao wanafunzi hao ni kuanzia cheke chea mpaka Chuo Kikuu.
Makundi mengine yaliyoombewani ni makundi ya wafanyakazi, Wafanyabiashara, Wafugaji, na Wagonjwa, Mara baada ya kutamatika kwa maombi hayo Mchungaji Dunia aliliombea taifa la Tanzania kisha akahitimisha kwa kuwaagiza wapiga vyombo wa kanisani hili kupiga wimbo wa Taifa ambapo waumini wote waliendelea kusimama juu na kuimba wimbo huo wa Taifa la Tanzania’Mungu lbariki Tanizani Mungu lbariki Afrika……..].
Baada ya kutoka kanisani hapo majira ya saa 7 usiku huku akiwa na baraka za Mungu kwa kushiriki lbada hiyo,Mwandishi wa Mtandao huu alipigia gia Pikipiki yake akaingia Mitaa mbali mbali ya Kata ya Mji Mpya na kushuhudia vituko vya ajabu vikiendelea Maeneo.
Baadhi ya matukio aliyoshuhudia Mwana habari huyo ni baadhi ya watu wakiporwa mikoba yao na Vibaka waliotumia mwaya huo wa kusheherekea Mwaka Mpya.
Eneo la Stend ya daradara ya Mji Mpya Mwandishi alishuhudia Vijana wakisomba takataka zilizokuwa ndani ya Viroba na kuzimwaga barabarani.
Masela wengine zunguka mitaani na Pikipiki zao kwa mwendo kasi huku boda boda hizo zikipiga kelele baada ya kuziburiwa ‘Exsos’ kwa Makusudi.
No comments:
Post a Comment