Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, January 1, 2024

INAUMA SANA. WAKAZI WA MAZIMBU WADAIWA KUTIRIRISHA TOPE LA KINYESI KITUO CHA WATOTO YATIMA.

Mstahiki Meya  Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro Pascal Kihanga.
Kinyesi cha tope kinachodaiwa kuelekezwa kwenye kituo hicho cha Mehayo
Mwandishi wa Mtandao huu akigawa zawadi ya nguo kwa watoto hao
                     Tope lingine likiwa eneo la kituo hicho



 


             Na Dustan Shekidele Morogoro.

MTANDAO Pendwa wa Shekidele unaoswasomwa na watu wengi Pande zote za dunia unawatakia Herry ya Mwaka Mpya 2024.

Leo January 1- 2024 tunaukaribisha Mwaka Mpya wa 2024 na kuuaga Mwaka 2023 kwa Stori hii ya kuhudhunsha.

 Baadhi ya Wananchi wa Kata ya Mazimbu Mkoani hapa wanadaiwa  kuerekeza Maji taka yanayotoka kwenye chemba za Vyoo vyao  na kuyaelekeza kituo cha Watoto wenye matatizo ya Viungo na Mtindio wa Ubongo cha Mehaya.

Malalamiko hayo yametokewa na Matron wa Kituo hicho Bi Esther alipofanya mahojiani Maalumu na Mwandishi wa habari hizi juzi.

Wiki iliyopita Desemba 25 2023 ilikuwa  kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Mwandishi wa Mtandao huu ambaye aliamua kutinga kwenye kituo hicho kusheherekea siku yake hiyo na watoto.

Mara baada ya kukamilika kwa sherehe hiyo iliyofanyika ndani ya ukumbi wa Kituo hicho, Mwana Birthday huyo aliingia kazini na kuzungumza na Matron akitaka kujua changamoto za kituo hicho. mahojiano hayo yalikuwa hivi.

Mwandishi. Naushukuru sana Uongozi wa Kituo cha Mehayo kwa kunipa nafasi ya kusheherekea siku yangu ya kuzaliwa na ndugu zetu hao wanaohitaji zaidi faraja zetu.

Matron. Asante sana  Mungu wa Mbingu akubariki kwa Moyo wako huo wa huruma ni wachache sana hapa duniani wenye moyo kama wako. kama ulivyoona watoto wamefarijika sana kwenye sherehe hii wame kula keki walioimis kwa muda mrefu.

Mwandishi. Hapa kituoni kuna watoto wangapi?

 

Matron.Tunajumala ya watoto na Vijana 45.

 Mwandishi.Kwa wiki wanakula kiasi gani cha Unga au mchele.

Matron.Kwa wiki Kama ni mchezo wakila Mchana na Usiku ni Kilo 50 kama unga pia kilo hizo hizo 50.

 

 

Mwandishi Mimi ni Mwandishi wa habari hivyo nageukia upande wa Pili wa Msaada nikihitaji kutumia kazi yangu ya Uandishi wa habari kusaidia kupaza sauti za changamoto zenu hapa kituoni mnakabiriwa na changamoto gani? Matroni. 

Changamoto ni nyingi lakini za muhimu tungepata Msaada wa Bima ya Afya kwa hawa watoto, changamoto nyingine ni Chakula kama ulivyouliza  watoto wako wengi hivyo chakula kinahitajika kwa wingi na mavazi pia.

Lakini changomoto nyingine inayotumiza ni hii ya baadhi ya Majirani zetu kuelekeza maji taka yanayotoka kwenye chemba za vyoo vyao  hapa kituoni kama unavyojua baadhi ya hawa watoto wanautingio wa ubongo wakikuponyoka tu wana kwenda kucheza kwenye hilo tope la kinyesi jambo ambalo ni hatari kwa afya zao,ukitoka hapo getini utaona tope hilo limepenya mpaka kwenye mlango na kuingia ndani, na huku pande wa nyuma ndio tope jeusi limepatakaka kwenye mrejeji likitoa harufu kali.

Mwandishi. Swali la Mwisho ukibahatika kuoanana na  Rais wetu Mpendwa Mama Samia utamuambia nini juu ya kazi hii unayaoifanya ya kuwarea watoto Yatima?.

Matroni. Nitamwambia anapofanya ziara mikoano akutane na wamiliki wa vitu vya  watoto yatima atasikia mengi kutoka kwa wamiliki wa vituo hivyo.

Mwandishi. Asante kwa ushirikiano Mungu atakubariki kwa kazi hii ngumu unayoifanya  sisi majumbani tunawatoto watatu au wawili heka heka zake ni kubwa, wakati mwingine usiku hatulali mara huyu ana homa mara huyu kafanya vile, kwako wewe unalea watoto hawa 45 wenye  umri tofauti kuanzia mwaka mmoja mpaka 22 si kazi rahisi barikiwa sana.

Matron. Amina na karibu tena.

Mwandishi, Asante  Mungu akinipa kibari cha kuniongezea mwaka mwingine Mwakani nitakuja tena hapa kusheherekea nanyi, Msiponiona basi jua Mungu ameutwaa uhai wangu kwani hapa duniani sote tunapitia kina nafsi itaonja Umauti.

Matron. Kwa Neema ya Mungu utafika tarehe hiyo tuna kukaribisha uje tena kuwapa faraja watoto hawa.

Mwandishi Amina.

 Muda huu Mwandishi wa Mtandao huu kamtwangia simu Diwani wa Kata ya Mazimbu Mh Pascal Kihanga ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Mji wa Morogoro  alipopokea simu moja kwa moja aliulizwa lshu yo ya tope la kinyesi majibu yake yalikuwa hivi.

”Shekidele kwa sasa niko nyumbani lringa nimekuja kula siku kuu na wazee wangu, swala hilo la baadhi ya wananchi kuelekeza maji taka kwenye kituo cha Mehayo ndio nayasikia kwako naomba nipe muda nilifuatilie na kama kweli lipo nitachukua hatua za haraka kulikomesha.

Binafsi ikupongeze kwa kazi nzuri unayofanya ya kuandika habari za kijamii nafuatilia sana habari zako.”alisema Meya huyo na kuongeza.

Kesho Jumanne naludi nikifika nitalifuatilia jambo hilo then nitakupa majibu sahihi.

 Nitumia nafsi hii pia kukupa Mwaliko wiki hii Mh Mkuu wa Mkoa atafanya ziara kwenye kata yangu ya Mazingu hivyo nakupa mwaliko rasmi uwepo kwenye ziara hiyo”alisema Diwani huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Morogoro’MRFA’

                         


No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...