Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, November 1, 2023

MCHANGANUA WA MASAA 24 YA WAZUNGU NA WASWAHIRI.


 Mzungu akispend juu ya Milima ya Uluguru akiangalia  Mandhari nzuri ya Milima hiyo.


              Na Dustan Shekidele,Morogoro.

KUNA siku nilikutana na rafiki yangu Mzungu, kwenye maongezi yetu tulizungumzia tamaduni zetu za kimaisha kwenye mataifa yetu kwa maana bara la Ulaya  na bara la Afrikai.

 Nilimpa nafasi awe wa kwanza kunieleza tamaduni zao alianza kwa kusema kwamba tamaduni zao wengi hupenda  kuzaa watoto 2 wakipangilia kisayansi mmoja wa kike na mwingine wa wakiume.

Kuhusu Chakula asubuhi wanakunywa chai nzito, mchana  chakula cha nguvu na usiku wanakula chakula raini kama vile chai na chapati za Maiya au Chips Kuku.

     MAHUSIANO YA KIMAPENZI.

”Kwetu sisi ukipenda umependa hakuna kificho, ndio maana mara nyingi unatuona tukitembea barabarani tunashikana mikono au kupigana mabusu ‘Pubric’ mfano katikati ya  soko au kwenye usafiri ya uma daladala.

 Never huwa hatusalitiani kwenye mahusiano na ikitokea mwenzio kabaini Umedet nje nasi hapo ndipo mwisho wa penzi, kwenye mahusiano yetu hakuna kosa kubwa kama kumsaliti mwenzi wako.  

      MGAWANYO WA MASAA 24.

Rafiki yangu huyo alimalizia kwa kunieleza wanavyoyatumia msaa 24 kwa siku 6 za wiki.

“Kwetu sisi masaa 24 tumeyagawa kwenye makundi 3, masaa 8 ya kwanza kwa maana ya saa 1 mpaka saa 8 mchana tunafanya kazi kwanguvu  kutafuta pesa.

Masaa 8 ya pili kwa maana ya saa 9 mchana mpaka saa 4 usiku tuna Spend ’kula bata.’

Msaa 8 ya Mwisho  kwa Maana saa 4 usiku Mpaka saa 12 asubuhi tuna lala hii ni kwa siku 6 jumatatu mpaka jumamosi, jumapili tunakwenda kanisani Kumuabudu Mungu”alisema Mzungu huyo.

IKAFIKA ZAMU YANGU KUELEZA UTAMADUNI WA KIAFRIKA.

Tunaanza na Chakula, baadhi yetu Chai tunakunywa saa 5 mchana baada ya baba wa familia kwenda shamba kuchimba mihongo. Chakula cha Mchana saa 10 na inategemea baba wa familia amejaliwa kupata chakula gani.

Chakula cha usiku  ugari ‘Dona’ Nguruka pembeni kuna kachumbali, ukimaliza kula unasukumia na Maji ya Kandolo.

                MPANGILIO WA UZAZI.

Baadhi ya familia zinafyatua watoto mpaka 10 huku wafamilia hiyo ikiishi nyumba ya kupanga .wakidai kila mtoto anakuja na riziki yake, kwenye swala la usaliti ndio usiseme mke wa mtu utamkuta anamiliki michepuko 4 na hii inatokana na ile mikopo yetu ya kausha damu na Vicoba.

Hapo kila Mwanaume anapewa jukumu la kulipia mkopo mmoja, huku Mume wa ndoa jukumu lake kutoa pesa ya kula nyumbani, Pia utakuta Mwanaume kipato chake kidogo lakini ameweka vimada wanawake wawili akiwalipia kodi za nyumba na kuwapa pesa ya kula kila siku.

            MGAWANYO WA MASAA 24.

Kwa tamaduni zetu baadhi yetu hulala masaa 3 au manne tu muda wote ni kazi, Mfano kuna rafiki yangu ameajiliwa kulinda mmoja ya soko la Manispaa ya Morogoro nyakati za usiku, anakesha kulinda mali za soko.

Mchana halali anafanya kazi ya pili ya kubeba mizigozi’Kuli’ bidhaa za wafanyabiashara wa soko hilo mfano maguni ya Viazi mvilingo na matenga ya Nyanya.

AU Shekidele mchana kutwa anatafuta habari Mtaani usiku anakwenda Mlala Nje kusaka matukio kumbi za starehe mpaka saa 8 usiku analala saa 9 usiku anaamka saa 1 asubuhi.        

                

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...