Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, September 30, 2023

BODA BODA ADAIWA KUMUUA UTINGO WA LORI KISA KIKIDAIWA KUWA MWANAMKE.

               Majirani wakimfariji mama kassimu
Bi Rehema Jacob  akihojiwa na Mtandao huu..
                   Marehemu kassim enzi za uhai wake

 Mwenyekiti wa Mtaa Said Jungu akizungumza na Mtandao huu nyumbani kwake.

 

              

 BODA BODA ADAIWA KUMUUA UTINGO WA LORI KISA KIKIDAIWA KUWA MWANAMKE.

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Dereva wa boda boda Omari Ngozi’ Maarufu  ‘Ommy Gunta’ anadaiwa kumuua  Kassimu Steven[23]ambaye ni utingo wa Lori kwa kumchomo tumboni na kitu chenye ncha kali huku chanzo cha ugomvi huo kikidaiwa kugombea mwanamke’demu’.

Tukio hilo ambalo kwa sasa ndio gumzo  mitaa mbali mbali ya Mji wa Morogoro limetokea Septemba 23 saa 4 usiku Kata ya Mji Mpya Mkoani hapa.

Baada ya mauaji hayo kutokea Mwananchi liliingia mzigo kukusanya taarifa zote muhimu A-Z.  

Mara baada ya mazishi  ya marehemu Kassimu yaliyofanyika Septemba 25 na kuhudhuriwa na umati mkubwa wawatu, siku iliyofuta Mwandishi wa habari hizi aliyeshirki pia Mazishi hayo, alitinga nyumbani kwa wafiwa Mtaa wa Fumilwa ‘B’ jirani kabisa na nyumba ya kina Asha Ngedere na kufanikiwa kuzungumza na Bi, Rehema Jacob ambaye ni Mama mzazi wa marehemu Kassimu.

Alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo kwa undani Mama huyo alianza kwa kusema.

“Siku nyingi Mwanangu aliniambia  Omar anamchokoza nikamwambia aende Polisi, Afande[anamtaja Jina]kamwambia ukimuona  amjulishe ili wamkamate.

Chanzo nasikia ni[anamtaja jina huyo Mwanamke] Shekidele wewe ni mwenyeji hapa Mji Mpya unafahamu kwamba ile nyumba yetu pale kwa wauza samaki kanunua mwenye Simba Oil na sisi tukainunua nyumba hii.

Hivyo huyo Mwanamke[anamtaja tena jina amepanga kwenye ile nyumba tuliyouza mara nyingi  mwanangu anapotoka  kwenye safari zake hupenda kwenda kupiga stori kwenye nyumba ile tuliyouza.

Nakumbuka siku ya tamasha la Muziki Mnene pale Jamhuri kundi la Vijana wa hapa Mtaani akiwemo Kassimu na huyo Mwanamke[anamtaja tena jina] wakati wanaludi nyumbani  usiku walikamatwa na Polisi kwa kosa la uzururaji siku iliyofuata waliachiwa.

Siku chache mbele Mwanangu  kaenda Dar kufanya kazi hotelini, hivyo ishu hiyo ya kumtafuta hakuifanya akawa bize na kazi, kama unavyojua hotelini wanakuja watu wengi hivyo kakutana na dereva wa Lori wamezungumka kampa kazi ya  utingo, hivi karibu karejea hapa Morogoro akawa anashinda kwenye kijiwe cha boda boda  pale kwa wauza samaki.

Juzi usiku nimefuatwa nikipewa taarifa zilizorarua moyo wangu kwamba  mwanangu amechomwa bisibisi  tumboni pake kwa Kapetera .

Nimejifunga kibwewe nimefika pale namkuta mwanangu amelala chini huku damu zikimvuja baada ya Muda mwanangu wa kwanza ambaye Mwezi huu ni Birdhday yake ya kutimiza miaka 23 amefariki dunia”alimalizia kusema  Mama huyo na kuangua kilio.

Juhudi za Mwandishi wa habari hizi za kumpata Omar ili azungumzie tukio hilo hazikuza matunda kufuatia mazingira ya tukio lenyewe badala yake alipatikana baba yake Mzazi Mzee Ngozi ambapo alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo na alipo mwanae alikuwa na haya yakusema.

“ Hadi sasa sijuia mwanangu alipo juzi Polisi walikuja nyumbani wamemtafuta hawakumpata wakaniomba niwasaidie kumtafuta nimepanda gari lao hadi shambani kwetu Mikese tumemtafuta pia hatukumpata, tumeludi hapa mjini tumempitia yule mwanamke anadaiwa kuwa chanzo tumeenda Polisi tumetoa melezo yetu.

Yule binti kaeleza vizuri sana kasema yule marehemu sio rafiki yake mtu wake ni Omar ambaye ndiye mwanangu, nasikia walipigana sana pale kwenye kijiwe cha boda boda kwa wauza samaki.

Marehemu baada ya kuzidiwa nguvu kafuata Panga kamtafuta Omar aliyeamua kuepusha shali na kwenda kijiwe kingine cha boda boda  pale kwa kapetela  kamfuata na kampiga panga kwenye paji la uso.

Kwa vile mwanangu ni boda boda anatembea na spana hivyo katika hali ya kujihamia na mashambulizi  kachomoa bisibisi kamchoma  tumboni”amesema Mzee Ngozi na kuongeza.

Inaniuma sana kila wakati nalia nikimkumbuka Mwanangu wa mwisho kindinda Mimba sijui yuko wapi na hilo jeraha”alimalizia kusema Mzee huyo ambaye kitaaluma ni fundi bonda.                 MASHUHUDA SASA.

Mwandishi wa habari hizi alitinga nyumbani kwa kapetera aliyetajwa  na wahusika wa pande zote mbili.

Mmiliki wa nyumba hiyo Bi Siwatu Kapetela alipohojiwa alisema” Shekidele mimi sijui chanzo cha ugomvi huo ingawa nasikia chanzo ni mwanamke hao watoto kassimu na Omar walianza kupigana pale juu kijiwe cha boda boda kwa wauza samaki.

Baadae ngumi hizo zikafika mpaka hapa walipofika hapo nje  kwenye kijiwe cha cha boda boda wamepigana hayo mapanga na kuchomana bisibisi, tumeshuhudia kassimu akiaunguka chini, watu wameenda kumwita mama yake alipofika kamkuta mwanaye yuko chini anavuja damu wamembena nasikia hawakifika mbali amefariki”alisema Siwatu Kapetera ambaye ni Mama Lishe kwenye nyumba hiyo.

 

       MWENYEKITI WA MTAA HUYU HAPA.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Fumilwa B Said Ally Ramadhan Jungu alithibithisha kutokea kwa tukio hilo.

“Ni kweli tukio hilo limetokea Septemba 23 majira ya saa 4 usiku chanzo kikitajwa kuwa ni mapenzi, binafsi kama kiongozi wa mtaa nilipata taarifa siku iliyofuata”alisema Mwenyekiti kiti huyo.

Alipoulizwa ana wito gani kwa wananchi wake  kuhusiana na  matukio kama hayo ya mauaji alisema.

”Shekidele hii inatokana na vijana wengi kukosa kazi za kufanya wanashinda vijiwe wito wangu vijana wafanye kazi naamini kama wangekuwa bize na kazi wasingepoteza muda kupigana mapanga eti kisa mwanamke”alimalizia kusema kiongozi huyo wa Mtaa.

Naye kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama alipohojiwa na Mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alithibisha kutokea kwa tukio hilo lakini akiomba Mwandishi afike ofisini  kwa taarifa zaidi.

RPC. Kweli tukio hilo limetokea lakini ziwezi kulizungumzia kwenye simu njoo ofisini.

 Mwandishi. Ok  nakuja hapo sasa hivi.

RPC. Niko safari  mpaka nikiludi.

                        

 

         


 

 

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...