Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, June 22, 2023

TAJIRI WA KIMASAI KUSHUHUDIA TAMASHA LA MORO KIDS LINAOUNDWA NA WACHEZAJI WA SIMBA, YANGA, AZAM

Tajiri huyo akizindua tamasha hilo kwaishara ya kupigw amkwaju wa Pelnaty
                   .......Akihojiwa na Waandishi wa habari
Vijana zaidi wa 200 wa taasisi ya Moro Kids wenye umri kuanzia miaka 8- 20

         Na Dustan Shekidele,Morogoro.

TAMASHA la awari la taasisi Maarufu nchini ya Kuibua na kukuza  Vipaji ya Moro Kids lililofanyika May 27 mgeni rasmi alikuwa tajiri Mainga Ole Kalaita anayemiliki taasisi ya kukuza na kuibua vipaji ya Tan Worriors  Soccar Academy yenye maskani yake Dakawa Wilaya ya Morogoro.

Tajiri huyo wa kimasai asiyena majivuni anamiliki pesa ndefu ambapo katika hali ya kuimalisha taasisi yake hiyo ya soka amefanikiwa kutembelea nchini zaidi ya 11 duniani ikiwemo nchi za Mabara ya Ulaya, Amerika Asia na Afrika.

Akizungumza kwenye tamsaha hilo akipewa heshima ya ugeni rasmi alisema kwenye ziara zake hizo za nje ya nchi amefanikiwa kupata marafiki kibao walioonyesha nia ya kukisapoti kituo chake hicho za kuibua na kukuza Vipaji.

Kesho kwenye tamasha  lililopangwa kufanyika Uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro, tajiri huyo wa Kimasai amealikwa.

Baadhi ya wachezaji nyota wanaotajwa kushiriki kwenye tamasha hilo ni pamoja na Dickson Job, Kibwana Somari, Zawadi Mauya, Mzamiru Yassin, na Shiza Kichuya, 

Wengine ni Hassan Kessy Kidingile. Salum Kihimbwa’Chuji’ Salum Kibaya, Hamad Waziri’Kuku’ Shomari Kapombe, Nickson Kibabage na lbrahm Ajib’Migomba’


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...