Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, June 19, 2023

HALI YA KUDUMISHA PENZI YA MBALI.


 


               Na Dustan Shekidele,Morogoro.

MPENDWA Msomaji wa Mtandao Pendwa wa Shekidele, nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ama baada ya salam tuingie kwenye somo letu pendwa la Mahusiano.

Leo somo hilo litadadafua vigezo muhimu vya kuliimalisha penzi la mbali,uzoefu unaonyesha wanandoa au wapenzi wanapotengana kwa kuishi mbali mbali kwa sababu maalumu kama vile majukumu ya kikazi, Kilimo, Maradhi na Likizi, penzi hilo huyumba kama sio kuvunjika kabisa  kwa sababu kuu moja ya kutoaminiana.

 Sasa leo tutajaribu kuelekeza  njia za kuimarisha mahusiano hayo ya mbali.

Mosi. Mahusiano ya mbali yanaihitaji hekima na utulivu wa hali ya juu huku ya kiimalishwa na Mawasiliano’Communication’ya mara kwa mara.

lsipunguea kupigiana simu mara 4 kwa siku, asubuhi kumpigia  mpenzi wako kujua ameamkaje, mchana kujua amekula nini, jioni kujua alivyoshinda Mwisho mpigie usiku.

Kwa wapenzi wa kweli muda huo wa usiku ndio muda mzuri wa kuzunguza kwa utulivu na kwa kirefu zaidi kwani muda huo kila mtu amemaliza kazi zake amejipunzisha sebreni au chumbani.

 Hapo mnauwanja mpana wa kuzungumza michakato ya kimaisha kwa lengo la kuinua kipato cha familia yenu  sambamba na kuimarisha uhusiano wenu huo wa mbali.

Mapenzi bila mawasiliano hakuna chochote ni kudanganyana tu hivi inaingia akilini unampenzi wako wa mbali halafu unakaa siku 2 au tatu hamjawasiliano kweli kuna mahusiano ya dhati hapo au ni kudanganyana?.

Pili- Penzi la mbali hata lile la karibu halipendi  mtu wa kulalamika lalamika kila wakati, wengi hawapendi lawama wanapenda furaha sio kitu kidogo tu mwanamke au mwanaume unamnunia mwenzio.

Mfano unampigia simu hapokei au hajibu sms unaanza kumuwazia mabaya. bila kujua sabau za yeye kutopokea simu,huenda  alikuwa mbali na simu au alikuwa kwenye usafiri wa boda boda simu iko kwenye pochi kwa wanawake au kwenye mfuko wa suluari kwa wanaume kelele za chombo hicho zimepelekea asiweze kupokea simu.

Ama eneo alilopo halikuwa salama kupokea simu kulikuwa na  vibaka kwa kweli kaiona simu yako lakini kwa usalama kamua kutoipokea,baada ya kuwa eneo salama kamua kukupigia na kukupa melezo hayo huelewi unamfokea.

 Elewa gubu ni kirusi kikali  sana kwenye mahusiano kina tafuna kwa kasi kubwa Upenzo kwenye mahusiano, gubu lingine halina kichwa wala miguu, kwenye mahusiano hayo hayo ya mbali mfano mkeo kaguaga nakwenda kwenye harusi umemkubalia katikati ya shughuri unampigia  kwa kukuheshima kaamua kutoka nje ya ukumbi mbio mbio kwa lengo la kupata utulivu wa kuongea na wewe.

Chaajabu unamfukoea na kumuawazi mabaya ukidai kwamba amekutapeli hayuko kwenye harusi mbona amechelewa kupokea simu nakwamba eneo hilo liko tulivu hasikie kelele za muziki. .

Mama wa watu anajaribu kujitetea kwamba kwa kukuheshimu kamua kutoka nje ya ukumbi bado hukubari unamwambia endelea na umalaya wako kisha unamkatia simu hii sio sawa.

Ninalolisema kwa wanaume nalisema pia kwa wanawake.uko mbali na mumeo unampigia simu hakupokea alikuwa akiendesha chombo cha moto kumbuka sheria za usalama barabarani zinazuia kuendesha gari, Bajaj au boda boda huku unaongea na simu.

 Hivyo baada ya nususa Mumeo kafika safari fasta kachukua simu na kukuta Mic Call za watu wengi ikiwemo yako na ya mama yake mzazi lakini kwa kukuheshimu anawapa kisogo wote kaanza  kukupigia wewe mkewe uliye mbali naye.

Unapokea simu hata  salamu hakuna unaanza gubu ukimuwazia mabaya kwamba alikuwa akikusaliti ‘baba umalaya utakuua umeona niko mbali unajisevia malaya  upendavyo na ukiwa nao simu yangu hupokei si ndio”mume anajitetea laakini mama huilewi umashusha mvua ya maneno ya shombo huku ukitishia kuvunja mahusiano yenu.

.

 

Kwenye penzi hili la mbali Kikubwa zaidi ni kuaminiana na kuheshimiana hata kama yuko mbali na macho yako mtunzie heshima yake ukijua kuna mtu  anayekupenda kwa thati, huku ukiwa na Tumaini  kwamba iko siku ataludi mtakuwa pamoja huku ikijifariji na maneno ya vitabu vitakativu vya Mungu vinavyosema Uvumilivu’Subra’ ni lbada.

Tatu- usipende kukusanya makosa ya mpenzi wako mara kwa mara,na kuyaweka kwenye moyo upatata shida kubwa ikiwemo magonjwa yasioambukizwa kama vile Afya ya akili, Presha, na kisukari, uwe mtu wa kusamehe kwani huyo mpenzi wako sio malaika ni binadamu aliyeumbiwa makosa hivyo ili kudumisha penzi lenu hamna budu kubebeana misalaba ya makossa.

Jenga  uaminifu kwa mwenzi wako tukumbuke binadamu tunapitia changamoto nyingi kama umeamua kuwa na mtu aliye mbali nawe jifariji kwa Imani kwamba ‘huyu mtu ni wa kwangu hawezi kufanya kitu cha kuumiza moyo wangu’Pia muombee kwa Mungu ampe moyo wa uaminifu .

Pia kuwa muwazi kwa mwenzi wako,hakikisha unapokwenda popote mjulishe huku ukimuaga kwamba mpenzi naomba ruhusa yako niende kwenye sherehe, au niende mjini kutembea.

Mwanamke unaweza ukawa mzuri sana, unashepu, rangi ya Mungu imekorea lakini tabia mbovu utajikuta unaachwa na wanaume mara kwa mara kwa kiburi chako na tamaa za mwili na pesa.

Hapa chini ya jua hakuna Mwanaume anawezesha kuishi na mwanamke mwenye tabia hizo, Kumbuka kila siku umri unasogea kadiri umri wako uavyosoge ndivyo na uzuri wako unavyozidi kupungua, ukipata mtu mwenye nia ya dhati ya kuishi na wewe kwa sasa mpe nafasi achana na mashoga wapotoshaji wanasema kuolewa ni utumwa.

Katika maisha naweza kusema kitu kinachoumiza zaidi moyo ni mapenzi hivyo kama unapata mtu anayekuumiza moyo wako mara kwa mara huwezi kuvumilia kuingia naye kwenye ndoa achana naye.

Kwa leo naishia hapa ikimpendeza Mungu tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine, kwa ushauri maoni wasiliana name kwa Whatspp namba 0715 28 90 73.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...