Thursday, June 29, 2023
KUMBUKIZI., MASHABIKI YANGA, SIMBA NA AZAM HAWAJAFIKIA VIWANGO VYA HAYATI YAMUNGU
Tuesday, June 27, 2023
MBILINGE MBILIGE ZA GEMU YA MASTAA WA SIMBA,YANGA NA AZAM
Shiza Kichuya akiitumikia timu ya Morogoro All Stars, dhidi ya Moro Kids All Stars, kwenye mchezo wa kirafiki wa kumbukizi ya Miaka 25 ya kuzaliwa kwa kituo cha kuibua na kukuza vipaji cha Moro Kids.
Gemu hiyo iliyopigwa wiki end iliyopita Uwanja wa Saba Saba Manispaa ya Morogoro imetamatika kwa Mastaa wa Morogoro Morogoro All Stars kupokea kichapo cha bao 1-0 Picha zaidi fungua profaili la Mtandao huu
Kichuya uso kwa Uso na Kipa hata hivo nyota huyo wa Namungo alishindwa kufunga bao baada ya shuti lake kukwada na kipa chukukizi wa Moro Kidss Geofrey Mmassa, Mmassa hajatoka bado yuko kwenye kituo hicho cha Moro KidsBeki wa zamani wa Simba na Yanga, Hassan Kessy 'Kidingile' ambaye kwa sasa anakipiga Dodoma Jiji huku tetesi zikidai msimu ujao atajiunga na Tabora United akidhibitiwa na beki wa Moro Kids All Stars.
Winga chipukizi wa Mtibwa Sugar aliyeitumikia timu ya Moro Kids All Stars Joseph Mkele[jezi no 8] akimiliki mpira huku akichungwa na beki wa Morogoro All Stars.
Winga wa Morogoro All Stars Jafar Kibaya[akijitwisha mpira kwa kichwa kwa lengo la kufunga bao huku Kipa wa Moro Kids All Stars Geofrey Mmassa akinyaka mpira huo na ukiweka salama timu yake,
lkumbukwe Kibaya ni mchezaji wa lhefu ya Mkoani Mbeya
Beki wa Mtibwa Sugar aliyeitumikia timu iliyoibuka kipaji chake ya Moro Kids All Stars Nassir Kombo 'Scobber' wakimdhibiti winga wa Morogoro All Stars.
Scobber akimiliki Mpira Picha zote na Dustan Shekidele,Morogoro
VITUKO VYA MWEZI JANUARI
Mwezi uliopita tumeshehelekea Siku Kuu mbili X Mas na Mwaka Mpya. Mwezi huu dume January tunashehelekea kulipa Ada za Shule na kod...
-
Mwandishi wa Mtandao akiwa juu ya Mlima Uluguru Mgeta Wilaya ya Mvomero Mwandishi wa Mtandao huu akiwa juu ya Milima hiyo ya Uluguru ak...
-
Na Dustan Shekidele,Morogoro. REHEMA za Mwenyezi Mungu na ziwe juu yenu wadau wote wa Mtandao Pendwa wa Shekid...
-
Morgoro Mji kasoro Bahari. ndiyo kauli ya Waluguru wa Mkoa wa Morogoro. Hii sio Meli na wala sio Uwanja wa Ndege 'Air Port' ni st...
