Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, April 8, 2023

TANZIA. MCHEZAJI WA ZAMANI WA SIMBA NA TIMU YA TAIFA AFARIKI DUNIA JIONI YA LEO.

                Marehemu Amri lbrahimu enzi za Uhai wake.

 Mwenyekiti wa Matawi ya Simba Mkoa wa Morogoro Said Mkweinda kulia akiwa na mtani wake Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga Mkoa wa Morogoro lssa Kitukwa[Maarufu lssa Chabala] ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Fumilwa B Kata Mji Mpya kwa leseni ya CCM waliponaswa na kamera za Mtandao huu hivi karibuni Maeneo ya Mji Mpya


              Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
Mchezaji nyota wa zamani wa Simba ambaye pia ni kocha Maarufu nchini na mchezaji wa kutumainiwa wa timu ya wachezaji wa zamani ya Moro Veterani Amri lbrahim amefariki dunia jioni ya leo.
 
Mtandao huu umepokea kwa masigitiko taarifa za kifo hicho usiku huu baada ya Mwandishi wa habari hizi kupigiwa simu muda huu wa saa 5 usiku na Mwenyekiti wa matawi yote ya Simba mkoani Morogoro Said Mkwinda.
 
” Shekidele mchezaji wetu wa zamni wa Simba Amri lbrahim amefariki dunia usiku huu hivyo mimi kama kiongozi wa matawi ya Simba nakupta taarifa hizi uzirusha pia kwenye mtandao wako”alisema Mkwinda ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Simu A Kata ya Mji Mpya Manispaa ya Morogoro kwa leseni wa CCM. 
 
Baada ya kupokea taarifa hizo muda huu Mwandishi wa Mtandao huu ambaye pia ni mchezaji na Mwanachama hai wa Moro Veterani aliingia kwenye Group la Watsap la Moro Veterani na kukutana na taarifa ya kifo hicho kisema. 
 
“Tanzia Mwalimu wa mpira wa Miguu na mchezaji wa zamani wa Simba Amri lbrahimu amekutwa amefariki nyumbani kwake Mungu amsamehe makosa yake yote.
 
Wana Moro Veterani tuliobaki Moro kesho saa 4 asubuhi tukutane pale Mochwari kufanya taratibu za kumsitiri mwenzetu” alisema taarifa kwenye Group la Moro Veterani. 
 
lfahamike timu ya Moro Veterani imeondoka jana kuelekea Arusha kwenye Bonanza la Pasaka linalojumuisha timu kutoka ndani na nje ya nchi. Kutokana na sababu Maalum baadhi ya wacheji wa Moro Veterani akiwemo Mwandishi na Mtandao huu waliomba udhuru hivyo hakusafari na timu. 
 
Enzi za Uhai wake Marehmu Amri lbrahim aliyekuwa akiishi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro aliwahi kuzichezea kwa mafanikio timu za Biashara Shinyanga, Simba ya Dar na Pamba ya Mwanza.na Reli ya Morogoro. Kabla ya kustaafu soko na kujiunga na mafunzo ya ukocha wa Soka. 
 
Baada ya kuhimu ukocha Marehmu Amri akiwahi kuzifundisha timu mbali mbali zikimo Polisi Moro kwa sasa Polisi Tanzania, Mkamba Rangers ya Kilombero iliyokuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza.
Burkina Fano ya Manispaa ya Morogoro iliyokuwa pia ikishiriki ligi daraja kwa kwanza. 
 
Hadi umauti unamkuta Amri lbrahimu alikuwa mwanachama wa Chama cha Makocha Mkoa wa Morogoro’TAFCA’ na Mchezaji wa Moro Veterani. 
 
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe, Tangulia Kamanda tutaonana baadaye.
 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...