Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, April 5, 2023

APRIL YA MWAKA HUU IMEJAA SIKUU KUU KIBAO IKIWEMO YA SIMBA NA YANGA.

 

Wachezaji nyota wa zamani wa Simba na Yanga wenyeji wa Mkoa wa Mwanza .

Huyu hapa ni Mrisho Ngassa wa Simba

                   Jorrson Tegete Winga wa zamani wa Yanga
                               Hayati Sokoine enzi za Uhai wake

 

Na Dustan Shekidele,Morogoro.

Hii inaweza kuwa stori ya kitaa. Mwezi huu wa 4 umejaa sikuu kibao uchunguzi nilioufanya muda huu kwa haraka haraka nimebaini mwezi huu wa 4 una sikuu kuu 9  rasmi kitaifa na zisizo rasmi.

 Siku kuu hizo ni ile ya Karume Day inayoadhimishwa April 7. Siku hiyo hiyo ya April 7 ni Good Friday[ljumaa Kuu] April 9 ni Easter Sunday[Jumapili ya Pasaka] na Easter Monday[Jumatatu ya Pasaka.

April 12 ni kumbukizi ya Kifo cha aliyekuwua Waziri Mkuu wa Tanzania Hayati Edward Morringe Sokoine.

lkumbukwe hayati Sokoine alifariki dunia kwa ajari ya gari April 12 1984 baada ya gari lake kugongana na gari lingine eneo la Dakawa Morogoro akitokea Dodoma akierekea Dar es salaam.

April 16 ni Sikuu kuu ya Simba na Yanga ambapo siku hiyo Wana robofainali hao wa michuano ya CUF watakipiga kwenye mchezo wa mzunguko wa pili ya ligi kuu Tanzania Bara.

Katika siku kuu zote hizo siku kuu hii ndio pekee yenye masharti ambapo sharti hilo ni la Mpaka mmoja wapo aibuke mshindi.

Hivyo dakika 90 za gemu hiyo ya watani wa jadi zitatoa majibu kama mshindi  ni Wananchi a.k.a Utopolo au Wana Msimbazi a.k.a Makolokolo.

April 21 au 22 ni Eid -El Fitri. April 23 ni Eid Pili yaani Eid Holday na siku kuu ya Mwisho kwa mwezi huu ni April 26 siku Kuu ya Union Day.   

            

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...