Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, February 15, 2023

VILIO VIMETAWARA JANA WALEMAVU WAKIADHIMISHA SIKU YA WAPENDANO DUNIA




      Mkurugenzi Mkuu wa MODICO akizungumza Jana
Kaimu Mkurugenzi wa MODICO akizungumzia lshu ya Ulawiti
                 Wali ndondo ukipelekwa ukumbini



 

 .

 .

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

lnasigitisha sana, baada ya Walemavu wengi kukosa Mialiko kwa Jamii yenye kipato kizuri kwenye siku kuu mbali mbali, jana sikuu ya wapendanao.’Valentine Day’Walemavua hao wameamua kuandaa sherehe ya kujipenda wenyewe.

 

 Walemavuo hao wamefanya hivyo  kupitia Umoja wao wa Morogoro Disability Devoroment and lmformation Centre[MODICO]  kwenye  siku hiyo Maalumu ya wapendao dunia ‘Valentine Day’ wakiwa na kauli mbio ya ‘Tarehe 14 Tone la Upendo’.

 

Kwenye Party hiyo Walemavu hao  wamejichangisha na kupika wali Maharage baada ya kukosa uwezo wa kununua Nyama na Vinywaji  Maji na Soda kama inavyoonekana kwenye meza kuu hakuna hata chupa 1 ya maji.

 

Kabla ya Walemavu hao kuonyeshana Upendo kwa kula pamoja Chakula hicho, Walipata wasaha wakuzungumzia Changamoto mbali mbali zinazowakabili wakiziwasilisha kwa Viongozi wao wa MODICO ambapo baadhi ya changamoto hizo ziliwaliza baadhi ya wanachama wa chama hicho walioshindwa kujizuia na kujikuta wakimwaga Machozi kama wanavyoonekana Pichani.

 

Miongoni mwa Changomoto iliowaliza kina bibi hao ni ile iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ya Maendeleo na Upashaji Habari Kwa Watu Wenyeulemavu[MODICO] Bi Stella Kisala[Pichani mwenye Blauz nyeusi Meza kuu] akizungumzia ishu ya Ulawiti kwa  Watoto wa kiume na Kike wanaowaongoza  Wazazi wao wenye Ulemavu  kuomba umba Mitaani nyakati za mchana na usiku.

 

Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MODICO  Bw Othuni Ngungamtitu akizungumza na Mtandao huu alisema” Sisi kama walemavu siku hii ya Valentine Day tumeandaa  party hii ndogo ya kujipongeza tukionyeshana Upendo wa kupendana sisi wenyewe baada ya kukosa mialiko kwa watu mbali mbali”alisema Mkurugenzi huyo na kuogeza .

 

 “Kimsingi umoja wetu  ni mchanga unawachama kama 50 hivi hatuna pesa  kwenye party hii tumejichangisha wenyewe tukisapotiwa na watu wenye mapenzi mema  wanaomiliki biashara zao za AfriMan. Zoeli. Nesi Gym na Tongenyama.

 

 Kipekee tunashukuru wewe Shekidele Umekuwa jirani sana na taasisi yetu ukifika mara kwa mara kwenye matukio yetu, tulipenda sana kualika Waandishi wengi wa habari lakini hatukuwa na fungu la kuwaalika tumekualika wewe pekee ambaye tunaujua Moyo wako umekuja kwa nauli yako tumekaa na wewe hapa kwa muda mrefu ukifanya kazi yetu bure bila kuhitaji ujira wowote kutoka kwetu.

 

 Mungu azidi kukubariki kwenye kazi yako na uendelee na moyo huyo huyo”alisema Mkurugenzi huyo ambaye aliwahi kuwa Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Pichani mwenye shati la damu ya Mzee meza kuu.

 

 Kwenye tukio hilo Mtandao huu umekusanya matukio kibao ikiwemo Walemavu hao kulilia kadi za Bima za Afya pamoja na Clip Video ya kaimu Mkurugrnzi wa ‘MODICO’ akizungumzia lshu hiyo ya Ulawiti iliyowaliza kina bibi hao.Hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote kuangalia Clip Video hizo.

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...