Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, February 12, 2023

LEO NI SIKU YA RADIO DUNIANI.

Mtangazaji Farham Abraham akiwahoji Wanamuziki wa Muziki wa Taarab

 Dustan Shekidele akiwajibika kwenye kipindi chake cha Fagio la Mtaa Planet Radio


LEO February 13 ni Madhimisho ya siku ya Radio dunia, Pichani Kaka na Dada wa damu wakiwajibika kwenye  kipindi cha Mcharuko wa Pwani Planet Radio yenye maskani yake  Ghorofa la Hotel ya Mount Uluguru  Mtaa wa Mlapakolo Kata ya Mji Mkuu Manispaa ya Morogoro.

 

Kwenye kipindi hicho Dustan Shekidele alimiliki kipengele cha Fadio la Mtaa akikusanya matukio mbali mbali Mtaani ikiwemo ya Udaku na kuyarusha kwenye kipindiki hicho kinachoanza saa 5 asubuhi mpaka saa 7 mchana Jumatatu mpaka ljumaa.

 

 Huku Farham Abraham yeye akimiliki kipengele cha Somo kwenye kipindi hicho akiwafunda watu mbali mbali wanaoteleza kwenye matukio mbali mbali ikiwemo ya Mahusiano ya kimapenzi, Kiudugu na Kiujirani.

 

 Kwa sasa Shekidele hayupo kwenye Radio hiyo huku Farham yeye akiendelea kuwepo akiwafunda watu kwenye Radio hiyo Pendwa Mkoani Morogoro inayoongozwa vyema na Madam Warda Makongwa.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...