Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, November 16, 2022

BABA MWENYENYUMBA ANASAKWA NA POLISI AKIDAIWA KUMCHOMA KISU MPANGAJI WAKE WA KIKE.

Vumia Pmari akumuonyesha Mwandishi wa Mtandao huu jereha hilo huku akiangua kilio kwa uchungu

                          Nyumba anayoishi Vumilia

                                                    RB No
 


 

Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 JESHI la Polisi Mkoa wa Morogoro linamsaka Bw Athuman Mohamed Aogwa akituhumiwa kumchoma Kisu Mpangaji wake wa kike Bi Vumilia Omari .

 

Tukio hilo la kikatili limetokea ljumaa iliyopita majira ya saa 2 usiku ndani ya nyumba hiyo iliyopo Mtaa wa River Side Kata ya Mwembesonga Mkoani hapa.

 

Jana Mtandao huu uriripoti kwamba Mapngaji huyo baada ya kusoma habari ya Udakuzi kwenye Mtandao huu alimpigia simu Mwandishi wa Mtandao huu na kumwalika kufika nyumbani kwake ili kumuelezea A-Z ya Mkasa huo Mwandishi wa habari hizi jana majira ya Mchana alitinga kwenye Nyumba hiyo na kufanikiwa kuzungumza na Mpangaji huyo ambaye amefunguka mazito.” Shekidele juzi ulivyokuja nilikwenda hospital baadae nikaenda Polisi nilipoka huko nikaenda kwenye Kikoba sio kwamba nimekukimbia kama ulivyoripoti kwenye Mtandao wako”alisema Mpangaji huyo aliyejitambuloisha kwa jina la Vumilia Omari.

Alipotakiwa kueleza tukio hilo alisema

 

”Siku ya tukio majira ya saa 2 usiku kwenye giza nene baada ya umeme kukatika Athuman kama kawaida yake ameludi akiwa amelewa nikamuliza kama amechukua sufulia yangu badal ya kujibu akanza kunitukana matusi ya nguo.

 

 Nilipomjibu kaingia chumbani kwake katoka na kisu akinikunja dera langu akataka kunichoma kisu tumboni Shemeji yangu Abdallaha anaye ishi humu ndani kamvamia Athuman na kumuambia huo ni udhaivu mtoto wa kiume kumpiga kisu mtoto wa kike”asema Vumilia na kuendelea kudadavua.

 

” Alivyoambiwa hivyo kataka kunichoma tumboni nikakikata kisu kwenye makali kakivuta kwa nguvu ndio kikanikata kwenye vidole hii kolido yote ilitapakaa damu.

 

 

 

 “ Baada ya kunichoma shemeji yangu kanipakia kwenye boda boda yake tukaenda Polisi nikafunguka kesi Kituo kidogo cha Polisi cha Mji Mpya na kupewa namba ya kesi MJP/ RB/144/2022 makosa Mawili Kujeruhi na kusa la Pili Lugha ya Matusi”alisema Vumilia.

 

Alipoulizwa  anaishi na mume kwenye nyumba hiyo Vumilia alisema anaishi  watoto wake 4 kwa muda mrefu baada ya  mumewe kutimkia  Moshi Mkoani Kilimanjaro kikazi.

 

Baadhi ya majirani walisikika wakisema Athuman na Vumilia kunakitu nimejificha chini ya kapeti kutokana na mazingia ya tukio hilo Vumilia alipoulizwa swali hilo alikana Vikali

 

”Sina mahusiano  yoyote na huyo Athuman  Mlevi wa kutupwa mimi nitampeleka wapi mpe leo laki 5 baada ya siku 2 hana hata senti tano, ninamume wangu nampenda  yuko mbali lakini huwa anakuja mara kwa mara”alisema Vumilia.

 

 Alipoulizwa swali la mwisho kwamba ameshaingia kwenye mgogolo mkubwa na baba mwenyenyumba wake kiasi cha kuchomana visu na kupelekana Polisi je mstakaba wake wa kuendelea kuishi kwenye nyumba hiyo ukoje? Alijibu.

“ Nyumba ziko nyingi ila akitaka kunifukuza kwenye nyumba yake ajipange kwa kunilipa pesa nyingi kwani kazi zangu natumia mikono naishi kwa kazi ya kusuka watu na kufua nguo kwenye majumba ya watu kwa sasa baada ya kunikata vidole siwezi kusuka wala kufua”alisema Vumilia kwa Jazba.

 

Juhuzi za Mwandishi wa habari hizi za kuzungumza na  Mtuhumiwa huyo ziligonga Mwamba kwa maelezi kwamba Mtuhiwa huyo anareja nyumbani  majira ya saa 6 usiku na kuondoka saa 12 asubuhi akikwepa kukamatwa na Polisi. Mtandao huu pia lifanikiwa kumreko Vumilia hivyo Clip Video za mahojiano hayo zitaruka hewani hivi Punde kwenye Mitandao ya Shekidele hivyo endelea kuwa jirani na Mitandao hiyo Muda wote.

                   

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...