Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Friday, September 23, 2022

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI,WANENGUAJI MAISHA MAPYA BAND WAENDELEZA MOTO WAO.

Mnenguaji Sabrina Danger ingizo jipya kutoka Waluguru Original akifanya yake




Josee Sembushe Vipi unaacha kupiga Bass unaangalia Tembo Falu

Mourine V.A.R angizo jipya kutoka Twanga pepeta akiruka hewani kama njiwa






Mnenguaji huyu namba Mpya akiwajibika jukwaani



         Husna Ramadhan a.k.a Mama Lao akifanya yake

 


       Na Mlala Nnje Dunstan Shekidele,Morogoro.

Wanenguaji Nyota wa band Pendwa ya Maisha Mapya ‘Wana Full Vipaji’ljumaa iliyopita wameuwasha mato mkali kwenye ukumbi mmoja uliopo pande za Mazimbu Manispaa ya Morogoro.

 

Mlala Nnje aliwashuhudia wananguaji hao wakipewa nafasi ya kucheza mmoja moja kwa lengo la kuonyesha Umahiri wao ambapo wapiga vyombo wa band hiyo waliwashushia Sebene zito wacheza shoo hao huku wakijazwa upepe na Rap wa band hiyo Abubakar Pugi.

 

 Aliyeanza kucheza alikuwa Sabrina Danger’Pichani’ ambaye ni ingizo jipya akitokea band ya Waluguru Original pia ya Mkoani hapa. Baadae akafuata Mourine V.A.R ambaye pia amejiunga na band hiyo hivi karibuni akitokea Twanga Pepeta ya Dar es Salaam.angalia fungu la Picha zake hapo chini kwenye Profaili la Mtandao huu.

 

Baadae alimalizia Mama lao Husna Ramadhan ambaye amejiunga na band hiyo akitokea band ya Extra Bongo pia ya jijini Dar es Salaam.

 

Kwa sasa watu wengi wanajazana kwenye shoo ya band hiyo kuangalia vionjo mbali mbali vikiwemo vya wananguaji hao wakali wa kazi hizo.

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...