Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, September 6, 2022

BAADA YA MZUNGU WA SIMBA MZUNGU MWINGINE WA KIKE AIBUKA MOROGORO






 


 

            Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

STORI ya Mjini kwa sasa ni ile ile ya letu Mzungu lete Mzungu, msemo huu umeibuliwa na Msemaji wa Simba Ahmed Ally siku ya kilele cha Simba Day alipokuwa akiwatambulisha wachezaji wa timu hiyo na siku zilizofuata mahasimu wao wamedukua sauti yake ya lete Mzungu na kuanza kumdhihaki.

 

Ilipofika zamu ya mchezaji mpya ya timu hiyo  Gedrolievic Dejan raia wa Sebria Msemaji huyo wa Simba amlimtambulisha Dejan kwa madaha zaidi ya wenzake akiseme.

“Lete Mzungu Lete Mzungu huyu ni Mzungu kweli kwelie sio Mzungu Pori”.

 

 Kama ilivyo desturi ya Watani wa jadi  waliibuka kwenye mitandao ya Kijamii wakiwakejeri watanizao hao kwa kutoa wimbo ‘lisong’ la lete mzungu lete mzungu wakidai  mzungu huyo hana Maajabu uwanjani na kwamba Simba wamepigwa kwenye usajiri huo.

 

Kwenye gemu ya ligi kuu kati ya Simba na Kagera Sugar Mzungu huyo alikata gebe za watu wote wanaobeza kiwango chake cha uchezaji baada ya kupiga bao la kideo.

 

 Wakati hayo ya Mzungu ya Simba yakiendelea. kwenye Masumbwi juzi Mzungu Mwingine  kumtwanga bondi wa Tanzania Hassan Mwakinyu usiku wa kuamkia juzi  jijini Lirvepool nchini Uingereza.

 

  Mwakinyo mwenye masikani yake jijini Tanga alitwangwa Round 4 alipohojiwa mara baada ya mwamuzi kuvunja pambano hilo kwa OK.Mwakinyo huku akiangua kilio alisema alisahau beg lake uwanja wa ndege hivyo alipewa viati vingine vilivyo mbana miguuni hali iliyosabaisha kupoteza pambano hilo.

 

Binafsi Mwandishi wa habari hizi anapinga utetezi huo kwa hoja kadhaa, Mosi mchezo hule sio wa mateke ni wamikono hivyo lshu ya viatua vya miguuni kumbana au kuto mbana havihusiani na ngumi za mikononi labda angesema Grops za Mkononi zinambana hapo angeeleweka kirahisi.

 

Pili wakati anahojiwa na Waandishi wa habari baada ya pambano hilo,nilimuona akiwa amevaa viatu hivyo hivyo alivyodai vinamdana na kumuumiza miguu, swali kama kweli viatu vilimumuzi mara baada ya pambano angevifua kuondoa hayo maumivu lakini hakufanya hivyo aliendelea kuvifaa.

 

Sisi tuliosoma Kiuba tunapata ukakasi wa kuamini utetezi huo, ni vyema angekubali kwamba Mzungu kamzidi uwezo kamtwanga kama yeye alivyowatwanga wapinzania wake huko nyuma ambao hawakuwa na visingizio walikubali kushindwa.

 

Tatu kama kweli viatu vilimbana awari angeomba pambani lisifanyike  mpaka apatiwe viatu vingine saizi yake, nakumbuka kuna siku Mwakinyo huyo huyo alipigana na Mzungu hapa nyumbani Tanzania.

 

Kabla ya pambano kuanza Mzungu huyo aligoma kupigana akishinikiza Yeye na Mwakinyo wabadilishe Grops zikaletwe nyingine Mpya, tunahisi huenda Mzungu huyo alihisi Grops za Mwakinyo zina Style ya Sakho zimenyunyiziwa mambo yetu yalee ya bibi na babu  kule Tanga ‘kamati ya Ufundi’.

 

Promoto wa pambano hilo kwa kushirikiana na waamuzi walikubali ombi la Mzungu huyo Mwakinyo alivua Grops hizo na kuvaa  mpya hata hivyo mwisho wa Siku bondi huyo asiyekuwa na Mpinzania Tanzania alimtwanga Mzungu huyo na kuwaziba midomo wale ‘Chawa’ walimdanganya Mzungu huyo kwamba Grops za Mwakinyo zimenyunyiziwa.

 

Sasa basi wakati habari za wazungu hao wa Simba na yule wa Mwakinyo  zikitamatika hivyo na hamia kwa mzungu wa Selous Morogoro Marathon, Mzungu wa kike aliyekimbia kilomita 10 kwenye mbio hizo, Mwandishi wa Mtandao huu akiwa na pikipiki yake ya mwendokasi alimfuatilia Mzungu huyu toka Mwanzosho wa mbio hizo zilizoanzia Viwanja wa Gofu na kuhitimishwa kwenye viwanja hivyo hivyo vilivyopo jirani na Morogoro Hotel.

 

Mzungu huyo alipokatiza mitaani watu wengi waliokutana naye walimwimbia wimbo wa Lete Mzungu Lete Mzungu hasa alipofika maeneo na Nane nane wimbo huo ulishika hatamu zaidi.

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...