Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, July 2, 2022

WAKUSHI FC MABINGWA MICHUANO YA PLANET NDONDO CUP MADIWANI WA PIGANA VIJEMBE.

Mwamuzi wa Ligi kuu Raphael lkambi maarufu Rapharl Webb[Mwenye Mpira akiziongozi timu kuimbia uwanja wa Saba saba jana
                           Kikosi cha Chadongo kilichoanza jana
KONGOLE KWENU. Kikosi cha Wakushi kilichoanza jana na kufanikiwa kutwaa ubingwa
Mc wa shughuri hiyo Salum Mapande ambaye [ia ni Mchambuzi Maarufu wa michezo katika kipindi cha Michezo cha Planet Redio akiwaamuru warembo kuliingia kombe uwanjani
 Kama mbele UEFA Champion....Warembo Ma Miss wakiliingia kombe uwanjani kabla mtanange huo kuanza jana


Karatasi zenye orodha ya majina ya wachezaji wa timu zote mbili

Mshambuliaji hatari wa Wakushi aliyewahi kuitumikia Stend United ya Shinyaka ilipokuwa ligi kuu akitafuta mbinu za kumtoka kiungo wa Chadongo Twalib Chachalo anayekipiga Petayose ya Tabora

Sehemu ya nyomi ya watu iliyofulika jana kwa kulipa kiingilio cha buku 2 getini
..Wachezaji Maras wakionyesha ubabe wa kukumbatiano wakisubiri mpira wa kona
...Mwamuzi akiwasuluihsiha wachezaji wakipigane kabali





Maafande wa voda fasta wakiongozwa na Afandne Clement Semizige Bazzo mwenye T-shirt nyekundu wakiwaondoa mashabiki waliosimama nyuma ya gori. ikumbukwe Bazo kabla ya kuajiliw ana jeshi la Polisi alikiwa mchezaji wa Reli ya Morogoro Simba na baadae Polisi Moro. kabla ya kusaafu soka na sasa kitambi kina mwagika



Kipa wa Chadongo ambaye pia ni Kipa wa Simba B akimkwatua mchezaji wa Wakushi nje ya 18
Cheki mshambuliaji wa Chadogo Colins Opere anaye kipiga Biashara ya Mara anavyokosa bao akiwa yeye na kipa


....Akijishangaa mwenyewe kukosa bao hilo huku akijiinamia kwa uchungu
"Kama wewe unacheza timu ya Ligi kuu na mimi nachezesha ligi kuu tena michezo ya timu kubwa inazozihusisha Simba na Yanga chukua kadi hii ya njano kwa kosa ulilofanya' hivyo anaonekna kusema Mwamuzi wa ligi kuu Raphael lkambi Webb akimlima kadi mchezaji wa Chadogo anayekipiga Biashara United ya Mara
Pongezi kwa kicha wa Chadongo Hussein Dior akipaa hewani kuoangua mpira uliokuwa ukiingia wavuni
Beki kisiki wa Chadongo Richard Joviti ambaye anakipiga moja ya timu kubwa za ligi kuu Zanzibar akimuingua Kipa huyo huku akimpongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya ya kupangua mpira ya juu. Richard ni Mkazi wa Chamwino Morogoro.



Mashabiki wakimbeba juu juu Beki 'Mkushi' Hassan Timbe baada ya kufunga bao hilo pekee kwa mkwaju ya adhabu ndogo nje ya 18
...Kipa wa Chadongo Dior akihangaika kudaka shuti hilo la Timbe na kujikuta akiingia nalo wavuni kama alivyonaswa na kamera za kisasa za Mtandao wa Shekidele, matuki kama haya ya chini ya Kapeti huwezi kuyapata popote zaidi ya kwenye Mtandao huu pendwa
kautema mpira huo umejaa wavuni hili ndio bao pekee lililoipa milioni mbili na kikombe timu ya Wakushi Fc
...Kwa furaha mashabiki wawakishi wamevamia uwanja kushangilia bao hilo lillofungadakika za lala kwa buriani
Mkuu wa Vipindi wa Radio Planet Madam Warda Makongwa akizungumza baada ya gemu hiyomya fainali kutamatika jana
Watangazaji wa kipindi cha Michezo Planet Fc Alen MwingiMpemba wa Chake chakeKushoto] aliyekuwa akitanga Mubashara mtanange huo kupitia masafa ya 87.5 Planet Fc na Mtangazaji Kiongozi wa kipindi cha Michezo wa redio hilo Jeska Mhagama wakimshikia vipaza sauti bosi wao wakati akijianda kumkaribisha mgeni rasm
Warda Makongwa akimkabidhi zawadi ya seti za jezi za waamuzi Mwamuzi Raphael lkambi
Mlezi wa timu ya Chadogo ambaye pia ni Mh diwani wa Kata ya Mkundi alipewa nafsi ya kukabidhi zawadi kw amshindi wa Pili aliyezawadi jseti moja ya Jezi na Pesa taslm laki 5 kutoka kwa waandiji wa kichuano hiyo kituo cha Redio Planet cha Mkoani Morogoro

Diwani wa Kata ya Mafiga Mchumngaji  Thomas Butabile
Diwani wa Kata ya Mkundi Mh Seiif Chomoka
Mgeni rasm Naibu Meya ambaye pia ni diwani wa Kata ya Saba saba akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi
Katibu Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Morogoro Ally Simba akizungumza baada ya kupewa nafasi jana
Mgeni rasm akimkabidhi Kombe Nahodha wa Wakushi Hassan Timbe ambaye pia nido mfungaji wa bao hilo Pekee
Wakushi wa mafiga , Misufini na Manzese mzuka umewapnda wakifanya yao na kigoma v=chao cha Ulugway huku maafande wakiwadhibiti wakifanya fujo
Mgeni rasmi akimkabidhi mfano ya check nahodha wa Wakuhsi Hassan Timbe
 


 

 

                           Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 

IMEISHA HIYO.

 

 

Wakushi Fc’Chuma cha Mjerumani’   kimegoma kuyeyushwa na badala yake kimewalaza njaa Mataji wa Chadongo Fc,iliyosheheni wachezaji wa Ligi Kuu kutoka timu za Polisi Tanzania, Ruvu Shooting, Biashara United na Mbeya kwanza.

 .

Timu ya Wakushi iliyoundwa na Vijana wengi wasio  na Majina Makubwa waliupiga mwingi na kuwafunika Mastaa hao na Chadongo na mwisho wa siku wakawachapa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali ya Michuani ya Planet Ndondo Cup ulipigwa jana Uwanja wa Saba saba Manispaa ya Morogoro.

 

 

Kwa ushindi huo Wakushi  kutoka Kata ya Mafiga inayounda Mitaa maarufu Morogoro ya Manzese, na Misufini wapokea zawadi za kombe  kubwa na Pesa taslimu Milioni 2 kutoka kwa mgen rasm Naibu Meya wa Manispaa ya Morogoro Mh Mohamed Lukwere

 

Bao hilo Pelee lililopeleka kilio kwa Chadongo limefungwa na beki wa zamani wa Mtibwa Sugar  Hassan Timbe dakika ya 81 baada ya kupiga faulo nje ya 18 iliyompalia Kipa wa Chadongo Hussein Dior akaitema na kujaa kwenye Net.

 

 Katika tukio la kushangaza Mshambuliaji wa Chadongo anayeichezea timu ya Ligi Kuu Biashara United ya Mkoani Mara iliyoshuka daraja juzi baada ya kukosa mabao amengi ya wazi aliamua kwenda kwenda banchi na kumuomba Kocha Wida widambe amtoe kwani aliamisi hakuna na siku nzuri kazini kwa siku hiyo ya jana.

 

 

Kocha huyo akatii ombi hilo na kumwingiza Abas Abas anayekipiga timu ya Polisi Tanzania ambapo naye hakuwa aliyekuwa na sumu kwenye timu hiyo alikuwa Abdul Maji Mengi anayekipiga Ruvu Shootin ya Mlandizi Pwani inayoshiriki pia ligi kuu.

 

. Mbali na Mgeni rasm Viongozi wengine mashuhuri waliohudhuria fainali hiyo iliyovunja rekodi ya wingi wawatu ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi’UVCCM’ Mkoa wa Morogoro Ally Simba.

 

 Mkurugeni Mtendaji wa Chuo cha Uandishi wa habari  mkoa wa Morogoro St Josephs College, Seif Chomoka  ambaye pia ni  Mh diwani wa Kata ya Mkundi ambaye pia ni Mlenzi wa timu ya Chadongo inayotoka kwenye Kata yake.

 

 

Wengine ni Diwani wa Kata ya Mafiga Mh Mchungaji Thomas Butabile aliyetinga uwanjani kuwasapoti Vijana wake wa Wakushi wenye maskani yao kwenye Kata yake.

 

Wakati wa kukabidhi zawadi kwa washindi Madiwani hao walitaniani Diwani wa Mafiga aliibuka na ubingwa alimtania diwani wa Mkundi ambaye timu yake ilichapwa na yeye kuambia kupewa heshima ya kuwakabidhi zawadi ya Mshindi wa Pili Vijana wake hao wa Chadongo.

 

 

 Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao likiwemo tukio la Sensea 2022 hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...