YEREMIA 29- 13
“Nanyi Mtanitafuta na kuniona, Mtakaponitafuta kwa Moyo Wenu Wote”
Hilo ndilo neno letu leo Jumapili ya Julay 3.
Kumbe Kupitia Maneno haya ya Mungu yaliyojaa faraja kubwa yanatukumbusha na kututia Moyo kwamba tutakapomtafuta yeye kwa Moyo wetu Wote tutamuona.
Lakini kumfikiea yeye ni safari ndefu inayohitaji Uadilifu endelevu, Upendo Usio koma. na Uvumilivu usio na Kikomo.
Kwenye safari hii utapita kwenye Milima na Mabonde, utakutana na changamoto Nyingi njiani zikiwemo za hatari lakini lengo lako liwe Moyo tu la Kumtafuta Mungu kwa Moyo wako wote,
ametuahidi kwa kufanya hiyo tutamuona Pasna shaka Yoyote.
Naamini kwenye safari hiyo kuna wengine watakutia Moyo na wengine watakuvunja Moyo wakiwemo watu wako wa karibu kama vile ndugu, zako wa damu, Marafiki zako wa ukweli, mke au Mume wako.
Mtumishi wa Mtandao huu anakuhusia na kuihusia nafsi yake pia, kwamba usiyumbishwe na hao watakao kuvunja moyo hata ikibidi kufanya maamuzi magumu ya tengana nao fanya hivyo kwa mahusiano mazuri na Muumba wako.
Kwa leo Uchambuzi wa Mtumishi wako unaishia hapam Mungu akipenda tukutane Jumapili ya Wiki ljayo kwa somo lingine.
Pichani Mmoja wa Viongozi wa dini Mkoa wa Morogoro akiiombea Pikipiki ya Mwandishi wa Mtandao huu aliyejitoa Mhanga kusafiri umbali mrefu na Pikipiki kwa lengo la kuwasaidi kupaza sauti kwa wanyonge waishio Vijijini.
Kwenye Safari hizo za Usiku na Mchana Mwandishi huyo anapita sehemu hatarishi kwenye maponde na Milima, Mara nyingine akikatiza kwenye Hifadhi zilizojaa wanyama wakali Kama vile Simba, Chui na Tembo akitafuta habari za kijamii za watu wanyonge waishio Vijijini wanadhurumiwa na kuonewa.
Pia kwenye safari hizo za Vijijini huripoti habari za kupaza sauti za wagonjwa wanaohitaji Msaada Serikalini na kwenye Taasisi Mbali mbali zikiwemo za dini na watu binafsi.
Baadhi ya gharama za safari hizo yakiwemo mafuta ya Pikipiki Mwandishi huyo akijikimu mwenyewe ikiwa ni moja ya sada zake kwa Jamii hiyo ya wanyonge.
“Hasara Roho Pesa Makaratasi, hakuna mtu aliyefirisiki kwa kuwasaidia watu wenye uhitaji”.
No comments:
Post a Comment