Na Mdakuz Dunstan Shekidele,Morogoro.
Jana Majira ya Mchana Julai 18 Mdakuz wa Mtandao huu akiwa kwenye Mishe Mishe zake kitaa akisaka matukio alipenyezewa udaku na Mwananchi mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
“Shekidele Mambo Vipi hapa sokoni kuna tukio, Mfanyabiasha wa Mwenzetu wa bucha la nyama amepata aibu ya Mwaka,tumeokota wallet lake likiwa na bonge la hirizi njoo uchukua Umbeya”alisema Mdau huyo mwenye jinsia ya kiume ambaye pia anafanya kazi kwenye moja ya mabucha ya nyama.
Baada ya kurambishwa Ubuyu huo Mdakuz alipiga gia Pikipiki yake ya Mwendo kasi na kutinga eneo la tukio ndani ya bucha hilo lililopo kwenye Moja ya Soko Maarufu Mkoani Morogoro.
Wakati zogo la kumshambulia mmiliki wa Walet hilo likiendelea Mdakuzi aliingia kazini kwa kufanya mahojiano na Shuhuda wa tukio hilo Msiki.
”Kama unavyojua sisi wafanyabiashara wa Nyama tunaamka alfaji saa 11 kwenda machichioni kuchukua Nyama na kuzisambaza kwenye mabucha yetu, sasa huyu Jamaa [anamtaja jina] alifika kwenye bucha hili la babu kaketi kwenye kiti usingizi ukampitia alivyokuwa akisota sota kwenye hiki kiti kinachokuchuka kama vile vya walemavu.
Walet yake aliyoiweka mfuko wa nyuma wa Jins yake ilianguka, alivyoamka kapanda boda boda kaenda kwenye bucha lake badae tukaokota Walet yake tulivyoikagua ndani turistaajabu tulivyoviona ndani.
Tulishuhudia shiringi elfu moja moja 5 Mpya pembeni ya hizo pesa tuliona hirizi nyeusi, huku katikati ya pesa tukashuhudia karatasi nyeupe yenye Maandishi ya kiarabu yenye rangi nyekundu.”alisema shuhuda huyo na kuendelea kumrambisha Ubuyu Mdakuz aliyezibua masikio yake kama Antena za Luninga.
“Kama unavyojua Wagogo wengi akiwemo mwenye hilo Pochi ni Wakristo tunajiuliza kajifunza lini kusoma Mandishi ya lugha ya Kiarabu,? tukajiuliza tena uwepo wa hirizi lengo lake ni lipi, Chuma Ulete au Mvuto wa wateja.?.
Baada ya masaa mawili hivi kapiga simu aliulizia Pochi yake tukamzunga kwamba tumeokota mapochi mawili hivyo ataje vitu vilivyomo kwenye Pochi yake ili tuweze kutofautisha tusije kumpatia Pochi ya mteja wetu.
Chaajabu kataja pesa elfu 5 hiziri na ile karatasi nyeupe kapata kigugumizi kutaja, tulivyozidikumchekecha kakata simu kuja hapa buchani na kuamsha zogo na sisi tumeshikilia msimamo wetu mpaka ataje vilivyomo ndani ndipo tumpatie Walet lake”alisema Shuhuda huyo.
Wakati tunakwenda Mitamboni tumepokea taarifa kwamba Mmiliki alikabidhiwa Walet yake ikiwa na vitu vyake vyote baada ya kujishusha akida kwamba hiziri hizo ni tiba ya maradhi yanayomkabiri na si za mvuto wa biashara wala Chuma ulete.
No comments:
Post a Comment