Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
USAFIRI wa boda boda umekuwa mkombozi Kwa watu wengi wa kipata cha chini hasa wale waishio Vijijini.
Mwandishi wa mtandao huu ambaye naye hutumia usafiri huo wa Booda boda kwenda Wilayani mbali mbali za Mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuripoti habari zinazowahusi watu wanyonge waishio Vijijini.
Mwanahabari huyo aliyejitoa mhanga kuwasaidi wananchi hao wa Vijiji kupaza sauti zao kwenye changamoto zinazowakabili.
Akiwa huko Vjijini Mwanahabari huyo amekutana na matukio mengine ya adha za usafiri na ubovu wa barabara.
Uchunguzi wa Mwandishi wa habari hizi kwenye safari zake za huko vijijini umebaini Usafiri wa Pikipiki Maarufu boda boda umekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wengi waishia maeneo hayo.
Mwandishi huyo wa habari za kijamii na kiuchunguzi alibaini usafiri wa boda bado hutumika kama gari la wagonjwa [Boda boda Ambulance Village] kusafirisha maiti kutoka kijiji kimoja kwenda kijiji kingine, pia huwakimbiza Wagonjwa wakiwemo wajawazito nyakati zote kwa maana Usiku na mchana kuwakimbiza vituo vya Afya.
Vile vile boda boda hizo hutumika kusafirisha Wanyama, Mazao hasa vyakati za mavuno pamoja na bidhaa za Madukani.
CAPTION
Picha no 1 Mwandishi wa Mtandao huu alimnana boda boda huyu akisafirisha maiti kutoka Moja ya Kijiji kilichopo Mpakati mwa Mikoa ya Tanga na Morogoro Kilindi Wilaya ya Kilongwe na Turiani Wilaya ya Movomero.
Picha no 2 Mwandishi wa Mtandao huu alimna boda boda huyu akiwa na Lumbeza za bidhaa za dukani akizisafiri kutoka Mnadani Kijiji ch Mlali Mgeta kuelekea dukani kijiji cha Vitonga.
Picha no 3 Boda boda alinaswa akisafirisha Mnyama Nguruwe .a.k.,a Kiti Moto haijafahamika mara moja alipotoka na anapoelekea kwa kwa sababua baada ya kusimamishwa na Mwandishi wa habari hizi aligoma kusimama.
Picha no 4 Mwandishi wa Mtandao huu akiwa moja ya Vijiji vya Mkoa wa Morogoro akitiza majukumu yake.
No comments:
Post a Comment