Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 4, 2022

BWANA HARUSI AFARIKI DUNIA MASAA 4 KABLA YA KUFUNGA NDOA.

Shehe Mkuu wa Kata ya Kichani Ally Kwembe akihojiwa na mtandao huu jana asubuhi juu ya kifo hicho
               Marehmu Ramadhani Rashid enzi za Uwahi wake
Msemaji wa familia Tausi Rashid dada wa Marehmu akihojiw ana Mtandao huu jana

 


 

                                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

 INAUMA SANA.

Fundi Maarufu wa  Vichwa vya Treni na Mabehewa kalakala Kuu ya Shirika la Reli Tanzania iliyopo Kata ya Kichangani Mkoani Morogoro, Ramadhan Rashid Mtakahela ‘Maarufu Tanna Best’ amefariki dunia masaa 4 kabla ya kufunga ndoa.

 

Kifo hicho cha ghafra na kuhudhunisha kilichoumiza mioyo ya  wengi, kimetokea June 30 Alhamis iliyopita  Majira ya saa 3 asubuhi, siku hiyo  Majira ya saa 7 mchana Marehemu aliyekuwa Mwalimu Mkuu wa Jogging Family,alipanga kufunga ndoa na Mchumba’ke Mpya kufuatia mkewe wa awari Mengi Ally kufariki dunia Januari 2020.

 

Marehemu Mtakahela  Jumatano iliyopita akiwa na afya njema alizunguka mitaani kugawa kadi za mwaliko kwa ndugu na jamaa zake,alifika pia nyumbani kwa baba yake mzazi Mzee Rashid maeneo ya Mji Mpya jirani na tawi kuu la Yanga kwa lengo la kuwapa Mwaliko Majirani wa mzazi yake.

 

 Mtakahela aliyekuwa pia rafiki wa Mwandishi wa habari hizi alikutana naye mitaani hiyo ya Mji Mpya na kumpa Mwalika.

 

”Shekidele kesho naoa karibu kwenye harusi Pia nitaomba unipige Picha kadhaa za kumbukumbu kwani harusi yangu haitakuwa na mbwembwe nyingi wala watu wengi’alisema Tanna Best ambaye kiasi ni mcheshi.

 

 Chaajabu siku hiyo hiyo ya ndoa Majira ya saa 5 mchana Mpiga Picha wa Mtandao huu akijiandaa kwenda kwenye harusi hiyo alipokea taarifa zilizorarua moyo wake kwamba Bwana harusi amefariki dunia.

 

 Mwandishi wa Mtandao huu hakuamini taarifa hizo hivyo aliamua kwenda  nyumbani kwa marehemu Mtaa wa Area 5 Kata ya Kichangani na kuamini baada ya kuona Turubani na umati mkubwa wawatu.

Kwa uchungu Mwandishi huyu hakufanya lolote zaidi ya kushiriki kwenye mzishi hayo ambapo ljumaa majira ya saa 10 jioni tulimpunzisha Mpendwa wetu kwenye nyumba yake ya Milele  makaburi ya familia yaliyopo Kingolwira.

 

 Jana Julai 3 Mwandishi wa habari hizi alitinga tena nyumbani kwa Marehmu kwa lengo ya kuripoti habari hiyo ambapo msemaji wa familia hiyo Tausi Rashid ambaye ni dada wa Marehemu alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.

 

”Ni kweli kaka yetu amefariki dunia ghafra Alhamis siku ambayo alikuwa afunge ndoa baada ya mkewe wa awari kufariki dunia mwaka juzi kama unavyoona  baadhi ya vyakula tulivyovianda kwenye harusi  ndio tunavipika kwenye msiba wake”alisema mwanafamilia huyo.

 

Alipoulizwa chanzo cha kifo hicho na marehemu ameacha watoto wangapi msemaji huyo alisema.

 

”Marehemu ameacha watoto 7 na wajukuu 10 na chanzo cha kifo chake kwa mujibu wa Mtoto wa marehemu  Mohamed anayeishi  hapa ni kwamba kila siku ratiba ya baba yake huamka alfajiri anaswali akimaliza kuswali saa 12 anakwenda mazoezi Jogging..

 

 “Mohamed amesema baada ya kuona mpaka saa 1 baba yake aliyekuwa amelala peke yake chumbani haja amka kamua kuingia chumbani  amemkuta anakoromo huku akitokwa na mapovu mdomoni.

 

 “Wakamchukua na kumkimbiza hospital  wakati madaktari wakiendelea kuokoa maisha yake kaka yetu alifariki duniani ,majira ya saa 3 asubuhi huku taarifa zikidai chanzo cha kifo chake ni Presha [Shinikizo la damu]”alifunguka msemaji huyo wa familia.   

            MENGI YAMESEMA JUU YA KIFO HICHO.

 Baadhi ya watu walikihusisha kifo hicho na mambo ya kishirikina, hivyo kufuatia hali hiyo Mwandishi wa Mtandao huu amezungumza na Shehe Mkuu wa Kata ya Kichangani Ally Kwembe ambapo alipotakiwa kutoa neno juu ya watu hao wanaozusha jambo hilo Sheikh Kwembe aliwashukia kwa aya ya mwenyezi Mungu.

 

 

Hata mimi nimesikia  mengi juu ya kifo cha Mtakahela nikili kupitia Mtandao wa Shekidele nikili kwa kinya kipana kwamba Marehemu alikuwa Muumini mzuri kwenye Msikiti wetu Mkuu wa Kata ya Kichangani.

 

 Hao wanazusha maneno hayo lmani zao ni hafifu Mandiko yanasema Kila Nafsi itaonja umautu na kila kilicho Juu ya Ardhi Kitatoweka.

 Niwatie moyo wafiwa wasisikilize maneno haya ya watu  wawe na subri ambayo kimsini ni lbada”alisema Shehe huyo ambaye ndiye aliyeongoza lbada hiyo ya Mazishi.

Alipoulizwa kama anamfahamu bibi harusi huyo aliyetaka kuolewa na marehemu Shehe Kwembe alisema

“Namfahamu vizuri  ni Mtoto wa Shehe Abdallah Msuko ambaye enzi za uhai wake kabla ya kifo chake aliwahi kuwa Shehe wa Msikiti wetu wa Kichangani.

 

Kwa dini ya kiislam sijuu hili limekaaje je kwa kuwa kila kitu kilikuwa tayari yalibaki masaa machache wanandoa hao wachome ubani na kuunganishwa kuwa mke na Mume je ile lbada ya eda inamhusu huyu Bi harusi au la?.

 

 Mtandao huu unafanya jitihada za kumtafuta Bi harusi huyo kusikia kauli yake juu ya kifo cha ghafra cha Mpendwa wake, hivyo endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.

 

 “Tangulia kamanda  tutaonana badae mbele yako nyuma yetu tutakukumbuka daima”

                   

No comments:

Post a Comment

AFANDE ANUSULIKA KIFO BAADA YA KUJIPIGA RISASI KISA MBWA ALIYEFUKUZA KIBAKA.

                                       Afande Ally Chinga       Na Dustan Shekidele,Morogoro. AsKARI Mgambo wa kampuni moja ya Ulinzi’...