Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
WAKATI msimu
wa ligi kuu Tanzania Bara, ukifika tamati leo, Uongozi wa Taasisi Maarufu
nchini ya kuibua na kukuza vipaji vya wachezaji ya Moro Kids ya Mkoani hapa,wameibuka na kudai Pesa
yao ya Usajiri wa Kipa mpya wa Yanga Abuutwarib
Msheri.
Majuzi Mwandishi wa Mtandao huu akiwa kwenye mishe mishe zake za kusaka
matukio alipigiwa simu na Mratibu Mkuu wa Taasisi hiyo Rajab Kindagule
akimwalika kufika kwenye taasisi hiyo.
”Shekidele tunajua Mtandao wako unawasomaji wengi, njoo hapa
Mazoezini kwetu Uwanja wa Shujaa tukupe habari inayomhusu Kipa wa Yanga Msheri”
Fasta Mwandishi wa
Mtandao huu alitinga eneo la tukio na Moja kwa moja Mratibu huyo alifunguka
haya.
”Kama taasisi tumekuita kutoa lalamiko letu ligi kuu inafika
tamati jumatano Mpaka leo Mtibwa hawajatulipa pesa yetu waliyomuuza Kipa Msheri
kwenda Yanga kama tulivyokubaliana kwenye mikataba yetu”.alisema Kindagule na
kuongeza.
Haya tunayaona siku
hizi lakini enzi la Uongozi wa Jamal tulikuwa tunalipwa haki yetu kwa wakati
wanapomuuza mchezji wetu wanatupa haki yetu, nakumbuka mzozo ulianzia kwa
Dickson Job tulihangaika sana kulipwa pesa yetu mpata tulivyowapeleka Mtibwa
Takukuru ndio wametulipa Malipo ya Job.
Kama taasisi tumeona
lalamiko letu tulipeleke kwenu Waandishi wa habari mtusaidie kupaza sauti”amemalizia
kusema Mratibu huyo ambaye ni Mwamuzi Mstaafu wa ligi Kuu Tanzania Bara.
Alipouliza Malipo hayo wanayoda ni kiasi gani, alisema
makubaliyao yao kwenye mkatani wa Kipa huyo ni kwamba atakapouzwa popote Moro
Kids watalipwa asilimia 25 ya pesa za mauzo.
Alipoulizwa swali la
pili kwa sasa taasisi hiyo ya Moro kids inawachezaji wangapi waliobaki kwenye
kikosi hicho cha Mtibwa kwa sasa. alijibu
“Tunawachezaji kama
watano hivi kwenye kikosi cha Mtibwa na kwenye kikosi chao cha pili asilimia 80
ya wachezaji wote wa timu B ya Mtibwa wanatoka kwenye taasisi yetu.
Baada ya kusikia malalamiko hayo jana Mwandishi wa habari
hizi aliwatafuta Viongozi wa Mtibwa kwa njia ya simu kwa lengo la kusikia kauli
yao juu la lalamiko hilo zidi yao.
Aliposomewa malalamiko
hayo na kutakiwa kuyatolea majibu Kiongozi wa Mtibwa aliyejitambulisha kwa jina
Moja la Abubakar alisema.
” Ni kweli Moro kids wanatudai hiyo pesa ila utaratibu
walioutumia wa kuja kwenu Waandishi wa habari binafsi sikuupenda na juzi tu
nimeongea na Kindagule nikimuomba waendelee kutuvumilia”alisema Kiongozi huyo.
Alipoulizwa kwa nini
wasilipe deni hilo ili hali wameshamuuza mchezaji huyo? Kiongozi huyo alijibu.
”Niwe mkweli Yanga hawajatulipa
pesa yetu ndio maana nikamwambia Kindagule aendelee kutuvumilia tulipipwa na
Yanga na sisi tutawalipa pesa yao”alisema Kiongozi huyo.
Alipoulizwa tena kwa
nini wamekubali kumtoa Kipa wao Muhimu bila kulipwa pesa ili hali wakijua
mchezaji huyo sio mali yao peke yao kuna taasisi iliyoibua na kukuza kipaji
chak.?
Kiongozi huyo hakujibu
swali hilo na badala yake alikata simu.
Siku za nyuma sakata hilo liliibuka kweny vyombo vya
habari ambapo Uongozi wa yanga urikaririwa ukidai kwamba umesharipa malipo ya
Kipa huyo na hawadai chochote.
Baadhi ya wachezaji wa Moro Kids waliotimkia timu mbali mbali
zikiwemo Simba na Yanga waliouzwa na Mtibwa Sugar ni Pamoja na Shomari Kapombe,
na Mzamiru Yasini Simba.
Dickson Job, Shomari
Kibwana na Kipa Abuutwarib msheri[Yanga] Shiza Kichuya, [Namungo].Hassan Kessy[KMC]
Juma Abdul Singida Big Stars na Hamad Waziri’Kuku [Mbeya City]