Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, March 12, 2022

UKATILI. NJEMBA AKAMATWA AKITAKA KUMBAKA DENTI WA DARASA LA KWANZA.KICHAKANI

Mtuhumiwa wa Ubakaji Said Ally akiwa amezima baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Wananchi wenye hasira Kali

....Akiwa Chini ya Ulinzi Mkali wa wananchi wakisubiri Polisi waje kumchukua
            Eneo aambalo dent huyo alitaka kubakwa na Njemba huyo
 


 

                         Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Wananchi wenye hasira kali wamemshushia Kichapo ‘hevi’ Said Ally ‘Maarufu Winga teleza’  Mkazi wa Mafiga Mkoani hapa, wakimtuhumu kutaka kumbaka Mwanafunzi wa kike jina linahifadhiwa kwa kuzingatia Maadili anayesoma darasa la kwanza shule ya Msingi Mwere.

 

Tukio hilo la kushangaza na kuhudhunisha limetokea juzi mchana kwenye Kichaka kilichopo jirani na shule hiyo.

 

Mara baada ya kutokea kwa tukio hilo baadhi ya wananchi walimtwangia simu Mwandishi wa Mtandao huu ambaye fasta alitinga eneo la tukio na kushuhudia jibaba hilo hivyo’ likitapakaa damu mwili mzito na ‘kuzima’ baada ya kushambuliwa na wananchi.

 

Akihojiwa na Mtandao huu mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo Jully Mushi alisema

”Mimi na huyu Jamaa yangu tulikuwa tuna toka Mji Mpya tunaelekea Mjini tukaamua kukatiza hii njia ya Relini ambayo kimsingi haitumiwi sana na watu kufuatia kujaa vichaka.

 

 Tulipofika katikati ya Kichaka jirani na Maghorofa ya Tumbaku tukashuhudia kelele za Mtoto, tuliposogea tukamshuhudia hii ‘Njemba’ akihangaika kumvua Sketi ya shule mtoto huyo akitaka kumbaka, alivyotuona akamuachia na kutimua mbia tukamfukuza tukafanikiwa kumkamata na kumshushia kichapo alivyozima tukamburuza na kumleta hapa shuleni pamoja Mwafunzi huyo”alisema Mushi. Akizungumza na shinda na Mtandao huu Njema huyo alisema

” Naitwa Said Ally nisamehe nimeteleza Pombe ndio iliyoniponza sitarudia tena” alisema Wimba huyo teleza akipachikwa jina hilo kwa tuhuma hizo za ubakaji.

 

Alipoulizwa kama ni Pombe kwa nini haikumtuma kwenda Kambi ya Machangudoa Pale Khahumba kununua wanawake wanaojiuza tena siku hizi wameshusha bei buku 5 utapata huduma. Mpaka Pombe hiyo ikutume  ukambake mtoto wa miaka 6 au umetumwa na wataalamu kwa lmani za kishirikina? Alijibu tena kwa ufupi ‘Hapana sio hivyo ni Pombe tu ndio maana naomba nisamehewe sitarudia tena”

 

Mtandao huu ulitinga Ofisi ya Mwalimu Mkuu kwa lengo la kupata ufafanuzi zaidi wa tukio hilo hapo  Mwalimu mkuu  wa shule hakuwepo na badala yake alikuwepo Mwalimu Mkuu Msaidizi.

 

Chaajabu alipotakiwa kuzungumzia tukio hilo aligoma.

”Siwezi kusema chochote kwa kuwa tukio hilo limetokea nje ya eneo la shule  huko vichakani sisi walimu hatuna tunachojua kazungumze na wananchi walioshuhudia tukio hilo ”alisema.  

 

Licha ya Mwandishi wa habari hizi kumbana Mwalimu huyo kwa kumueleza kwamba tayari ameshazungumza na Wananchi hao anahochotaji ni kauli ya Uongozi wa shule kuhusiana na tukio hilo. ticha huyo mwenye jinsia ya kike aliendelea kushikilia msimamo wake wa wa kukwepa kuzungumzia tukio hilo.

 

,Msimamo wa Ticha huyo ni kinyume na Maagizo ya Uongozi wa juu wa Serikali wa kuwataka watendaji wote wa serikali kutoa ushirikiano kwa Waandishi wa habari pindi wanapohitaji taarifa kutoka kwenye maeneo yao.

 

 Baadaye Difenda lilitinga eneo la tukio likamchukua Mtuhumiwa huyo pamoja na dent huyo ambaye awari alifichwa ofisi ya Walimu na alipotolewa nje na Polisi baadhi ya wananchi  walishindwa kujizuia na kuangua Vilio kutokana na udogo wa dent huyo anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 6.

 Jana asubuhi Mwandishi wa habari hizi alitinga Polisi kwa lengo la kuzungumza na  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Musilim,kamanda huyo hakuwepo  alikuwa  nje ya ofisi kikazi.

 

Majira ya 9 Alasiri Mwandishi wa Mtandao huu alimtwangia Simu RPC huyo  ambapo alipokea msaidizi wake” Bosi yuko kwenye kikao simu zake ninazo mimi msaidizi wake akitoka nitamwambia akupigie”alisema Bodgard huyo wa RPC.

 

Hadi habari hii inaruka hewani Mwandishi wa habari hizi hajapokea simu kutoka kwa Kamanda huyo.

 

Clip Video za tukio hilo yakiwemo Mahojiano na Mtuhumiwa huyo zitaruka hewani hivi punde kwenye YouTube ya Shekidele.

                  CAPTION.

Mtuhumiwa akiwa chini ya Ulinzi wa Wananchi huku akiwa amezima kwa kichapo. Picha no 3 eneo la Kichaka ambapo tukio hilo limetokea.

Kuna njia nyingi za kupitia ambazo hazina Vichaka lakini huenda kwa njaa dent huyo aliamua kujiripua na kukatiza peke yake kwenye kichaka hiki ili awahi kufika nyumbani kwao na kwa bahati mbaya amekumbana na seke seke hiyo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...