Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, March 12, 2022

UJUMBE WA NENEO LA MUNGU LEO JUMAPILI UNATOKA MWANZO 3-1-19



 

 MWANZO 3 1-19

Bali nyoka alikuwa Mwerevu  kuliko wanyama  wote  wa Mwitu aliyowafanya Bwana Mungu akamwambia Mwanamke atii hivi ndivyo alivyosema Mungu Msile Matunda ya Miti yote ya bustani.

 

Mwanamke akamwambia nyoka Matunda ya Miti ya bustanini twaweza kula.

Lakini matunda ya Mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema msiyale  wala msiyaguse msije Mkafa.

 

 Nyoka akamwambia Mwanamke hakika hamtakufa. Kwa Maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayo kula  Matunda ya Mtii huu  mtafumbuliwa Macho  nanyi mtakuwa kama Mungu mkijua Mema na Mabaya. Mwanamke alipoona ya kuwa ule Mti wafaa kwa Chakula wapendeza Macho,nao ni Mti wa kutamanika kwa Maarifa basi alitwaa katika matunda yake akala akampa na Mumewe  naye akala.

 

 Wakafumbuliwa Macho wote wawili wakajijua kuwa wa Uchi, wakashona Majani  ya Mtini,wakajifanyia nguo.Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu ikitembea bustanini wakati wa jua kupunga.

Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.  Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia uko wapi?.

 

Nasikia sauti yako bustanini  nikaogopa kwa kuwa mimi ni Uchi nikajificha.

 

Akasema ni nani aliyekuambia ya kuwa U-uchi? Je umekula wewe matunda ya Mti niliyokuagiza usiyale?.

 

 Adamu akasema huyu Mwanamke uliyenipa  awe pamoja name ndiye aliyenipa  matunda ya mti huo nikala. Bwana Mungu akamwambia Mwanamke nini ili ulilolifanya?.Mwanamke akasema nyoka alinidanganya nikala.

 

Bwana Mungu  akamwambia nyoka kwa sababu umefanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote na kuliko hayawani wote  walioko Mwituni kwa tumbo utakwenda na mavumbi utakula siku zote za maisha yako.

 

Nami nitaweka uadui  kati yako na huyo Mwanamke  na  kati ya uzao wako  huo atakuponda kichwa na wewe utamponda kisigino.

 

Akamwambia Mwanamke hakika nitakuzidishia uchungu wako na kuzaa kwako kwa uchungu utazaa watoto  na tama yako itakuwa kwa mumeo naye atakutawala.

 

Akamwambia Adamu kwa kuwa umesikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza nikasema usiyale.

 

Ardh imelaaniwa kwa ajiri yako  kwa uchungu utakula  mazao yako  siku zote za maisha yako. Michongoma na miiba itakuzalia nawe utakula mboga za kondeni.

 

Kwa jasho la uso wako utakula chakula hata utakaporudia ardhi ambayo katika hiyo ulitwaliwa kwa maana u mavumbi wewe  nawe mavumbini  utarudi.

“Hilo ndilo neno letu la leo Jumapili ya March 13.ambalo linatufundisha tutii maagizo ya Mwenyezi Mungu na tuache tamaa za Mwili na Mali”. Mwendelezo wa stori ya Njemba anayedaiwa kumbaka dent wa la kwanza itaendelea kesho leo tumempa Mungu utukufu wake  tukikumbushana Mandiko yake.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...