Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, March 16, 2022

KIGOGO NMB BANK ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAPIGA PICHA MOROGORO.

Kigogo wa NMB Hamis Ulanga akihojiwa na Mwandishi wa Mtandao huu huku akiwa na Kamera yake.
Kigogo huyo wa NMB akifungua Kikao cha  Mkutano Mkuu wa dharura wa Chama Cha Wapiga Picha Morogoro

Katibu Mkuu Njovu akielezea mafanikio na Changamoto Mwaka 1 wa Chama hicho.
Wanachama wa Umoja huo wakiwa kwenye kwenye Picha ya Pamoja Jana akiwemo Mpiga Picha wa Mtandao huu mwenye T-shirt nyekundu Kushoto.

 


                                Na Dunstan Shekidele Morogoro.

 KIGOGO Mstaafu wa NMB Bank tawi la Jamhuri Road Bukoba Mkoani Kagera Hamis Ulanga  hivi karibuni amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Wapiga Picha Morogoro.

 

Mzee Ulanga  aliyekuwa bosi wa kitengo cha ldara ya fedha za Kigeni[Foreign Exchanger Dep] tawi hilo baada ya kustaafu alihamia Mkoani hapa na kujiingiza kwenye ujasiliamali ambapo alinunua Kamera na kuwa Mpiga Picha za Mitaani akipiga picha kwenye hafra mbali mbali kama vile Kitchen Party, Send Off na Harusi.  

 

Kigogo huyo wa NMB alitumia usome wake kuwakomfisi Wapiga Picha kuanzisha Chama na kukisajiri Serikalini, baadhi ya wapiga Picha akiwemo Mpiga Picha wa Mtandao huu walikubali wazo hilo na kulifanyia kazi.

 

January  Mwaka jana walifanikiwa kuanzisha chama hicho ambapo March 7 mwaka Jana walipata Usajiri namba 2062 Serikali ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.

 

Chini ya Uongozi wa Msomi huyo wa Uchumi na Fedha  kutoka NMB Wapiga Picha hao walisajiri Umoja  huo kwa jina la Uluguru Mountain Photographers Of Morogoro’UMPM’

 

.Akizungumza kwenye Mkutano Maalumu wa kutimiza Mwaka Mmoja wa Chama hicho uliofanyika jana Katibu Mkuu wa Chama hicho Washinton Njovu’ Maarufu Marekani’ alisema Mpaka sasa Umoja huo unawanachama 39.

 

”Chini ya Uongozi wa mwenyekiti wetu tumefungua Acount Bank kupitia michango ya wanachama tunapesa taslimu zaidi ya laki 7 Bank ikiwa ni michango ya wanancha kwa Mwaka mmoja”.

 

Tulikusanya Pesa zaidi ya hizo lakini tulitumia kwenye shughuri  mbali mbali kama vile kuwapa Pesa wanachama waliopata Misiba na wengine kupata maradhi au kuuguliwa na wapendwa wao”alisema Njovu na kuongeza.

 

Lengo la Umoja  ni kukusanya Pesa nyingi zaidi ili tuweze kukopesha wanachama wajikwamue kiuchumia”alisema Katibu huyo anayeongoza Umoja huo kwa Weledi.

 

Mpiga Picha wa Mtandao huu ni Miongoni mwa wanachama waanzirishi wa Umoja huo aliyekataa uteuzi wa Uongozi kwa sababu mbali mbali zikiwemo za kuwa kiongozi kwenye  Vyama Vingine.

 

lfahamike Mpiga Picha wa Mtandao huu ni Mwanachama wa Chama cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro, Mwanachama wa Chama cha Wasambaa Mkoa wa Morogoro, Mwanachama wa timu ya Morogoro Veterani, Mwanachama wa Band ya Muziki ya Maisha Mapya,Mwanachama wa Umoja wa wafanyabiashara wa Soko la Kihonda Mazimbu Road, pia ni Mwanachama wa Jumuiya ya KKKT Sayuni Nane nane Tubuyu. Wanawane wanaweza Mwanamke Pekee wa Umoja huo ameganya jambo lake habari na Picha za tukio hilo zitaruka hewani hivi Punde.                                                 

 

 

 

 

 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...