Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, December 22, 2021

KUMBUKIZI.

Mwinjilisti wa kanisani la KKKT Kitunda Dar akiongoza lbada fupi ya kumuombea Marehemu ndani ya Hospital ya Amana kabla Mwili wa Mpendwa wetu kusafirishwa kuelekea Lushoto kumpunzisha kwenye nyumba yake ya Milele.

 Pichani Bibi Kette akinipa wosia kwa Lugha ya Kisambaa kwenye moja ya sherehe zake za kuzaliwa’Happy Birthday iliyofanyika nyumbani kwake Moshi Baa


 Na Dunstan Shekidele,Dar es salaam

Leo Desemba 22 Mpendwa wangu. Mke wangu, Kipenzi cha  Moyo wangu, barafu wa Moyo wangu, My Number One, Mshauri wangu, Msili wangu  Kette Abdallah umeniacha mpweke baada ya kutwaliwa na Bwana akiwa usingizini nyumbani kwako  Gongolamboto,Mombasa, Mtaa wa Moshi Baa jijini Dar es salaam.

Marehemu Kete  ambaye ni bibi yangu aliyenizalia Mama yangu Mzazi alifariki dunia Desemba 22 2019 akiwa na umri wa Miaka 103.

Marehemu ameacha watoto watatu Tumaini Samwel Juma, ‘Mrs Shekidele’, David Samwel Juma na Neema Samwel Juma’Mrs Mulokozi’ Wajukuu, Vitukuu na Vilembwe zaidi ya 100.

 

Leo Desemba 22 2021 ametimiza miaka 2 toka alivyofariki dunia na kuzikwa kijijini kwake Mlalo Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga

Kesho kuna stori ya Kero za Mtaa itaruka hewani hivyo,baada ya stori hiyo kesho kutwaa Mwendelezo wa Stori hii ya bibi kete pamoja na Picha zaidi zikiwemo za  Clip Video  za mahubiri ya Mtumishi wa Mungu akimmwagia sifa bibi huyo eneo la hospital ya Amana jijini Dar zitaruka hewani hivyo nakusihi usikose matukio hayo.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...