Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, December 23, 2021

KERO YA MTAA. WANAOPIGA PINI MAGARI WALALAMIKIWA NA UPENDELEO.

Gari la kwanza kupigwa Pini saa 5 na dakika 32 angalia kwenye Picha saa na na tarehe.

Mita kama 30 mbele takribani dakika 3 mbele gari hili la serikali liliegesha sehemu isiyo ruhusiwa kisheria, wakamataji walipouna ni la serikali walilipita hawakulikamata.

Dakika 4 mbele baada ya kuliacha gari la serikali walimekamata gari hili huku dereba akiw andani ya gari kama anavyoonekana Pichani akiwaomba msaada wakamataji hao bila mafanikio

 


Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Wiki iliyopita baadhi ya madereva wa Magari binafsi Mkoani hapa, walitoa kero yao kwa Mtandao huu wakilalamikia kitengo kilichopewa jukumu la kusimamia alama za barabarani kwa kuyakamata na kuyafunga Nyororo Magari yote yanayokiuka alama za Usalama barabarani ikiwemo kuegesha Magari maeneo yasiyoruhusiwa’Long Paking’

 

 Lalamiko kuu la Madereva hao wanadai wahusika wanaufanya kazi hiyo kwa Upendelea kwa kuyakamata magari ya watu binafsi huku yale ya serikali yanayovunja sheria wakiogopa kuyakamata.

Baada ya kupokea Malalamiko hayo Jana Mwandishi wa Mtandao huu aliingia kazi kufanya uchunguzi wa malalamiko hayo kama yana ukweli au la.

 

Majira ya Mchana Shushu wa Mtandao huu alitinga katikati ya Mji wa Morogoro akawaona Wakamataji hao wakiwa kwenye Bajaj yenye rangi nyeusi, Shushu  akiwa kwenye Pikipiki yake ya Mwendo Kasi akaifuatilia Bajaj hiyo kwa nyuma kila ilipokatiza.

 

Mara paa Bajaj hiyo ikasimama barabara ya Madaraka jirani na Msikini wa wahindi ‘Jamati’wakashuka na kuipiga Cheni gari iliyoegeshwa  eneo lisiloruhusiwa.

 

Kweli dereva huyo alistahili kukamatwa ambapo licha ya uwepo wa alama ya kuzuia kuegesha gari eneo hilo  alikaidi na kupack gari lake na kuondoka zake kufanya shoping za X Mas Madukani.

 

Uwepo wa gari hilo eneo hilo kulisababisha usumbufu kwa madereva wengine sambamba na foleni kwenye barabara hiyo yenye msongamano mkubwa wa magari hasa nyakati za jioni.

 

 Kwa vile muhusika hakuwepo kwenye gari hilo  Mabaunsa hao walilipiga pini kasha wakaondoka zao,Shushu wa Mtandao huu baada ya kupiga Picha gari hilo fasta akapiga gia Chombo yake na kuendelea na uchunguzi wake  kwa kuendelea kukifuatilia Kibajaj hicho.

 

Chaajabu mbele kidogo takribani mita 50  toka lilipofungwa gari la kwanza kulikuwa na gari la Serikali ambalo pia limeegeshwa eneo lisiloruhusiwa bila kujua kama wanafuatiliwa na Shushu Wakamataji hao walipunguza mwendo  Kibajaj chao wakalitazama gari hilo baada ya kusoma namba na kubaini ni gari la serikali waliliacha wakaondoka zao.

 

Mita 30 tena wakakuta gari binafsi limeegeshwa eneo lisiloruhusiwa huku dereva wa gari hilo akiwa ndani ya gari amewasha End keta Double Azad wakalipiga pini.

 

Mzee aliyekuwa ndani ya gari hilo kwa hekima aliomba Msamaha huku akijitetea kwamba aliegesha mbele ya duka lake kwa dakika chache ashushe mzigo,  Mabaunsa hao hawakumsikiliza badala yake waliendelea kulipiga cheni.

 

Baada ya ombi lake kukataliwa Mzee huyo alishuka kwenye gari akazama kwenye duka  lake hilo la Vifaa vya Shule na Maofisini’Stationery’ akavuta droo akakunya elfu 50 akalipa Cash faini hiyo wakamfungulia.

 

Mwandishi wa Mtandao huu aliwafuata Mabaunsa hao na kuwaeleza “Makamanda Mambo Vipi hongereni mnafanya kazi nzuri baadhi ya madereva walikuwa wakiegesha hovyo magari utakuta kulia mwa barabara kuna gari zimeegeshwa, kushoto mwa barabara hivyo hivyo, hali hiyo husababisha folezi zisizo za lazima kwa watumiaji wengine wa barabara.

 

Mimi kama Mwandishi wa habari nilipokea malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba kazi yenu mnaifanya kwa upendeleo kwa kukamata magari ya watu  binafsi huku yale ya serikali mkiyaacha, mfano hapo nyuma mita kama 30  kuna gari la serikali  mmeliona hamkulifunga mpaka sasa naliona lile pale bado lipo tena kwenye kibao cha No Paking”.

 

Walijibu kwa Mkato ‘Kanunue cheni ukalifunge wewe”baada ya majibu hayo ya shombo wakapiga gia Kibajaj chao wakaondoka zao.

 

Mwandishi wa Mtandao huu aliingia kwenye Stationery na kuzungumza na Mzee huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la  Buruhani Manyisa Maarufu Mzee Manyisa.

 

“ Yaani nimesimama kwa dakika kama 1 au 2 nikiwa ndani ya gari kama ulivyonipiga Picha nimewaita Vijana wangu wanipokee hili boksi la karatasi mara na stuka gari langu linafungwa, licha ya kujitetea sana  Vijana wale hawakunielewa.

 

Nilikata kwenda kwenye Kibajaj chao kuzungumza nao nikawaita hapa mbele za watu nikalipa cash faini elf 50 nika changia mapato ya serikali yangu”alisema Mzee Manyisa ambaye ni Mstaafu wa Jeshi la wananchi wa Tanzania’JWTZ’.

 Kufikia hapa shushua wa Mtandao huu alikamilisha kazi aliyotumwa na wananchi na imeifanya kazi hii kwa welezi kwa takribani dakika 20 tu na kubaini Magugu na Ngano Mchele na Pumba Maji na Mafuta.

Angalia Picha za magari matatu tofauti mawili ya watu binafsi yamepigwa Pini na Moja la serikali limeachwa huru

 

lli kudhibitsha hili na kuondoa makando kando Mwandishi wa Mtandao huu aliamua kuseti kamera yake Tarehe na Saa kama inavyoonekana inavyosomeka kwenye Picha hizo.

 

Hivi karibuni baada ya magari ya serikali kudaiwa kuendeshwa kwa Mwendokasi na kusababaisha ajari na kuuwa watumishi wengi wa serikali Viongozi mbali mbali wakiwemo Mawaziri walikemea jambo hilo huku wakiwaagiza Askali wa kikosi cha Usalama barabarani kuwakamata madereva wa magari ya serikali wanaovunja sheria.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...