Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Thursday, October 21, 2021

MORO VETERAN MABINGWA WA BONANZA LA NYERERE DAY.

Profesa Matundo Mtambo[Kati]  Mh Diwani wa Segerea [kulia]na kushoto ni nahodha wa Moro Veterana Seleman

                   Kikosi kabambe cha Moro Vwrweani

 


 

                             Na Dunstan Shekidele.

 

BAADA ya kutwaa ubingwa wa bonanza la UMSOTA lililofanyika wiki iliyopita mkoani Morogoro, timu kabambe ya Moro Veteran Jumamosi iliyopita imetwa tena ubingwa wa bonanza la Nyerere Day lililofanyika Mtaa wa Toto Tundu Segerea Mwisho Jijini Dar es salaam.

 

Moro Veteran wametwaa  ubingwa wa bonanza hilo lililoshirikisha timu 8 baada ya kuzitandika timu zote saba zilizo cheza na Wababe hao kutoka Mji Kasoro bahari.

 

Mara baada ya kutwaa ubingwa huo Mgeni rasmi wa bonanza hilo Mh Diwani wa Kata hiyo alimkabidhi kombe na seti ya jezi nahodha Msaidizi wa Moro Veteran  Mluguru Selemani ambaye naye baada ya kupokea seti hiyo ya jezi alimkabidhi Mlezi wa Moro Veteran Profesa Madundo Mtambo.

 

Jumapili Mchana Mabingwa hao wa kihistoria  waliingia kwenye Coaster yao  na kurejea Mkoani Morogoro na zawadi zao huku  Maveterani wa Dar wakikokodolea machozi wabeba wao wakitimka zao na zawadi hizo.

 

Baada ya kutoa dozi kwa timu hizo za Dar Moro Veterani wamepata Mwaliko wa kwenda Zanzibar kwenye bananza lingine litakalofanyika Desemba. , bonanza hilo lililoandaliwa na UMSOTA ni Maalumu kwa uzinduzi wa Kanda ya 9 ya Zanzibar.

Kama kawaida panapo majaliwa ya Mwenyezi Mungu Mwandishi wa Mtandao huu ambaye pia ni Mchezaji hatari wa Moro Vetetani atakuwepo kwenye bonanza la Zenji.  


 

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...