Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, September 15, 2021

HAPPY BIRTHDAY MH -SHABIBY

Mh Shabiby kulia akiwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari Mkoa wa Morogoro Nikson Mkilanya akimpongeza Mhe Shabiby kwa kufanikiwa kuongeza Mwaka Mwingine.
 


 Na Dunstan Shekidele, Morogoro.

 Leo Septemba 15 ni kumbukizi ya kuzaliwa ya mbunge wa Jimbo la  Gairo mkoa Morogoro Mh Ahmed Shabiby ambaye kwa kibali cha Mwenyezi Mungu leo amemuongezea mwaka mwingine.

 

 

 Jamii ya wana Morogoro tuna mengi ya kuigwa kutoka kwako, licha ya kuwa Mfanyabiashara mkubwa, ukibeba pia Cheo cha kuchaguliwa na Wana Gairo cha Mbunge

 

 Hadi leo Unaishi nyumbani kwako Wilayani Gairo tofauti na baadhi ya waheshimiwa wengine wakipata mafanikio kidogo wanahamia Dar, kubwa zaidi licha ya utajiri ya Utajiri wako una baya na watu watoto wakileo wanasema hujimwambavai, kwa Maana Unamajivuno, hulingi na wala huna dharau kwa watu wote wakubwa kwa wadogo mafukala na Matajiri.

 

Mh Shabiby akikujua ndio kabisaa hawezi kukupita, juzikati nikiwa maeneo ya Msamvu jirani na Stend ya Mabasi ya  Mikoani nikiwa kwenye Mishe Mishe zangu niliona gari la kifahari V8 Shangingi linasimama mbele yangu.

Nikastuka nikiwa kwenye mshangao niliona Mh Shabiby akifungua kioo cha gari na kunisalimia na baada ya salamu kama kawaida yake akanitani.

 

” Shekidele uko ba baiskel boda boda yako umeuza nini”alisema Mh Shabiby ambaye baada ya kusalimiana aliingia kwenye hotel yake Mpya ya kisasa ya Ghorofa Nane iliyopo Jirani na Stend ya Msamvu.

 Katika kudhibitisha hilo wakazi wa jimbo la  Gairo wataniunga mkoni ambapo tajiri huyo anawajua karibu wote wakubwa kwa watoto, Zaidi ya yote ni mpenda maendeleo na anatamani kila mtu akuwe kiuchumi kama yeye.    

 Mafanyabiashara mwingine ambaye licha ya utajiri wake na Ubunge wake hakuhama Morogoro ni Mhe Aziz Abood                                              


No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...