Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Saturday, August 14, 2021

WAKUSHI FC MABINGWA WA THE GUNNERS NDONDO CUP 2021.

Kikosi cha Wakushi Fc Kilichotwaa Ubingwa wa The Gunners Super Sixsteen 2021
                                    Kikosi cha Chadongo 
 Winga hatari wa Chadongo Abdul Seleman Sopu' ambaye kwenye mcihuano hii ya ndondo ameonyesha kiwango kizuri sana ama kwa hakika Coastael Unioni inayoshirik ligi kuu mtu
 Beki wa Wakushi Fc  Muddy Katoto anayekipiga Polisi Tanzania yenye Maskani yake Moshi Kilimanjaro
                Manahodha wa timu zote mbili wakiwa na waamuzi
Mkuu wa Vipindi vya Michezo Planet Redio Choi Stevan[mwnye barako akiongoza meza kuu kwenda kukagua timu jana jioni
Mwamuzi wa hakima Raphael lkambi Webb' akisalimiana na Mwenyekiti wa Waamuzi Wilaya ya Morogoro 

Mwandaaji Mkuu wa Michuano hiyo Seleman Mpemba akisalimiana na wachezaji wa timu zote mbili



Wamekamilisha kazi ya kukagua timu ujumbe huo ukielekea meza kuu
Hapashika nguo kuchanika uwanjani kuwania kiticha cha Milioni Moja




Nyomi ya watu iliyofulika jana kushuhudia gemu hiyo kw akiingilio cha buku 2 geni
Line One Dismas ambaye pia ni Mshikakibendera bora wa ligi daraja la kwanza msimu uliopita akiwajibika jana kwenye fainali hiyo ya Ndondo Cup



 Beki kisiki wa Wakuhsi Nassoro Chollo[kulia] akimdhibiti winga hatari wa Chadongo Abdul Sopu ambaye anakipiga Coastal Unioni ya Jijini Tanga, Chollo anakipiga Mawenzi Marketi ya Mkoani hapa



 Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

 

WATOTO wa Mujini Wazee wa Mipango Wakushi Fc yenye Maskani yake Makutano ya Mitaa ya Manzese na Misufini katikati ya Mji wa Morogoro jana wametwaa ubingwa wa michuano bora ya The Gunners Ndondo Cup ‘Super Sixsteen’ 2021.

 

Wakushi inayoongozwa na Chacha Marwa ilimetwaa ubingwa huyo kwenye mchezo wa fainali uliopigwa jana uwanja wa Saba saba, baada ya kuinyuka Chadongo Pelnaty 5-4 kabla ya kufika kwenye hatua hiyo ya Mikwaju wa Pelnaty dakika 90 za awari miamba hiyo ilitoka sale ya bao 1-1.

Mara baada ya gemu hiyo iliyokuwa tamu kwa muda wote wa dakika 90 Mgeni rasm wa mchezo huo Mwanamichezo bora mkoani Morogoro ambaye pia ni diwani wa Kata ya Mkundi na CEO wa Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro’MSJ’ Mh Seif Zahoro Chomoka aliwakabidhi zawadi washindi kitita cha pesa taslimu million Moja huku mshindi wa Pilia akiambulia laki 5.

 

 Kama kawaida Mtandao huu umekusanya matukio kibao kwenye gemu hiyo yakiwemo za makabidhiano ya zawadi kwa washindi na wachezaji bora akiwemo Kipa bora wa Simba na Mfungaji bora wa Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...