Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Sunday, August 15, 2021

DIWANI AMTAJA SAMATA KWENYE FAINALI YA NDONDO CUP.

Mgeni Rasmi Mh Seif Chomoka akimkabidhi kiticha cha Milion Moja Nahodha wa Wakushi Fc Muddy Katoto ambaye pia ni beki kisiki wa Polisi Tanzania
Mh Chomoka akihesabu kitita hicho cha Pakeji ya Milion Moja
Nahodha wa Chadongo akikabidhiwa zawadi ya Mshindi wa Pili Laki 5 Cash
                       ....Wakihakikisha kiasi hicho cha pesa
 Mwenyekiti wa Chama cha Waamuzi Wilaya ya Morogoro akimkabidhi zawadi ya Kadi Nyekundu, ya Njano na filimbi refa bora wamichuano hiyo Fikiri Magari. Msimu wa mwaka juzi Magari alipanda daraja na kuchezesha ligi Kuu kabla ya msimu uliopita kushuka daraja 
Mkuu wa Vipindi vya Michezo Planet Radio Choi Stevenkushoto] akimkabidhi zawadi ya  Glops Mpya Kipa wa Chadongo Hussein Dior ambaye aliibuka Kipa wa bora wa Michuano hiyo.

Hussein Mkazi wa Dumila Morogoro ni Kipa wa kutumainiwa na Simba B ya jijini Dar. lkumbukwe katika story za nyumba Mtandao huu uliwahi kuripoti kwamba Kipa huyo ameonyesha uwezo mkubwa kwenye kila mechi aliyodaka

Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Morogoro Anthony Muhando[kulia] akimkabidhi zawadi ya Peya Moja ya Viatu Vipya Richard Mwamba wa Wakushi Fc aliyeibuka Mfungaji bora wa Michuano hiyo akiwa ametupia mabao 6 kwenye michezo 3 yaani ule wa Robo fainal Nusu fainali na fainal. 

'Rich' ni mchezaji wa kutumainiwa na  Mtibwa B ilioyotwaa ubingwa wa Ligi kuu ya Vijana chini ya Miaka 20' Under Twent'

Nahodha wa Wakuhsi akimkabidhi kitita cha Milioni Moja Katibu Mkuu wa Wakushi Faraji
Mratibu Mkuu wa The Gunners Ndondo Cup Seleman Mpemba

Mh Chomeka]kushoto' akiteta jambo na Mratibu Mkuu wa Michuani ya Ndondo Cup Seleman Mpemba.


 

                 Na Dunstan Shekidele,Morogoro. 

DIWANI wa Kata ya Mkundi Manispaa ya Morogoro Mh Seif Zahoro Chomeka,amemtaja Mtanzania anaye cheza soka la Kulipwa Ulaya Mbwana Samata kwenye Michuano ya The Gunners Ndondo Cup’ Super Sixsteen 2021.’

 

Mh Chomeka aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye  fainali hiyo aliyasema hayo kwenyen hotuba yake kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi

 

 “ Fainali hii kati ya Wakushi na Chadongo ilikuwa nzuri sana nawapongeza Chadongo kushika nafasi la Pili lakini pia nawapongeza Wakushi kwa kutwa ubingwa huu.

  Kwa ukubwa wa soka lililopogwa hapa zawadi ya hazitoshi hivyo mimi naongeza zawadi bingwa aliyeandaliwa kupaya milioni moja namuongeza laki 3 kwa hiyo na mshindi wa pili aliyepata laki 5 namuonge laki mbili.

 Ndugu zangu mpira kwa sasa ni ajari nzuri Kijana Mwenzetu Samata kwa sasa ni tajiri sana kwa sababau ya Mpira Mguu wake unamlipa pesa nyingi” alisema diwani huyo ambaye pia ni Mmiliki wa Chuo cha Uandishi wa habari Morogoro’MSJ’  

Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mh Chomoka alisema Msimu ujao wa michuano hiyo anaongeza nguvu ya zawadi ili kuzidisha hamasa kwa wachezaji ambapo alisema Michuano hiyo inalengo la kuibua vipaji vya Vijana wa Kata zote 29 za jimbo la Morogoro ikiwemo kata yake ya Mkundi

 Mratibu wa michuano hiyo Selemani Mpemba ambaye ni Mtoto wa Makamo wa Pili wa Rais Mstaamu  wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibae Mh Balosi Seif All ldd alisema Michuano hiyo iliyoanza June 21 na kutamatika juzi Agost 13 ilikabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo cha baadhi ya timu kuchelewa kufika uwanja hali iliyopelekea baadhi ya michezo kulala baada ya giza kutanda uwanjani wakati timu hizo zikiwa sale.

 

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...