Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Wednesday, August 4, 2021

THE GUNNERS NDONDO CUP, WAKUSHI FC YATINGA FAINALI KIBABE.

Winga wa Wakushi Fc Gira akishangia kwa Style ya Morrison baada ya kupachika bao la 3 huku akipongeza na wenzake, alifanya hivyo mbele ya mashabiki wa Nughutu Fc


       Kikosi cha Wakushi Fc Kilichosheheni wachezaji Waluguru
Kikosi cha Nughutu Fc kilichosheheni wachezaji raia wa Ghana
Baadhi ya wachezaji wa Nughutu raia wa Ghana wakipozi mbele ya kamera ya kisasa ya Mtandao huu yenye uwezo wa kupiga Picha 10 mfurulizo kwa sekundi 5.kwa umbali hata wa mita 300.
...Cheki beki wa Nughutu Salum a.k.a Ali Ali akimdhibiti kira mafanikio Richard ambaye kwenye mchezo huo alipiga bao 2 peke yake. ifahamike Richi ni mchezaji wa Mtibwa B huku Salum akikipiga Lipuri ya lringa ambapo kabla ya kutimkia Lipuli Saluma alikuwa akiitumikia timu ya Maafande wa 515 KJ ya Kinonko Bwawani Morogoro Vijijini. 

Wanajeshi hao ndio Mabingwa wa ligi daraja la 3 mkoa wa Morogoro kwa misimu 2 mfululizo. Hivyo Wajeda hao walipokwenda lringa kwenye Michuano ya FA Maarufu Azam Federation Cup Lipuli walivutiwa na kiwango wa Mchezaji huyo na kuamua kumsajiri.

                  ...Salum akimpiga roba Richard
         ....Rich akachomoa kabari akiendelea na safari zake




.... Baada ya kabari kuferi Salum beki kisiki akimchapa Mtama Rich baada
KUFUKEANA. Beki wa Nughutu Sepepa akifokeana na Mwamuzi Ally Mnyumbe ambaye pia ni Refa wa Ligi kuu Tanzania Bara
Michuano ya The Gunners pia inatoa fursa kwa wafanyabiashra ambapo Mama huyu akigonga shoo kali ya kuuza Uji ya Urezi na Mchele kama anavyoonekana Pichani akizingira na mashabi wakigombea Uji huo ambapo kikope kimoja ni jero
 Baadhi ya Mashabiki walioshuhudia Michuano hiyo ya The Gunners kwa kiingilio cha buku 2
Mrembo huyu naye Shabiki wa Msimbazi akitembeza biashara yake ya Visheni uwanjani hapo
Winga hatari wa Wakushi Mrisho Said 'Ziko wa Kilosa' akigombea Mpira na beki wa Nughutu Fc

Mapacha wasioachana kwenye safari zao Doto na Kubwa masela wangu kutoka Pande za Vibandani Kata ya Mbuyuni kwa Mh Diwani Samwel Msuya wakipozi mbele ya Mtandao huu" Shekidele na sisi tutwange Picha ukaturushe kwenye Blog yako' walisema Mapacha hao wawili Mashabiki lia lia wa Black Viba ya Vibandani.

Kipa wa  Nughutu Joris Kamen akipuyanga na kuruhusu bao la kwanza lililopachikwa na Richard umbali wa mita 45

 


                      Na Dunstan Shekidele,Morogoro.

Timu ngumu ya Wakushi Fc yenye Maskani yake Mitaa ya Misufini na Manzese Kata ya Mafiga Mkoani hapa, imekuwa timu ya kwanza kutinga fainali ya Michuano ya The Gunners ndondo Cup’Super Sixsteen 2020-21’ baada ya juzi kuindandika timu bora ya Nughutu Fc kutoka Bong’ora Kata ya Kilakala kwa bao 3-1.

 

 Kabla ya mchezo huo mashabiki wa timu hizo walitambiana vikali ambapo Nughutu ilitapa kuitandika Wakushi kwa kile walichodai wamesheheni wachezaji wengi wa Kigeni kutoka nchini Ghanam huku mashabiki wa .Wakushi nao wakitamba kwamba wataibuka washindi kwa vile timu yao imejaa wachezaji Waluguru kutoka Kinole na Matambo.

 

Hadi dakika 45 za awari zinakamilika timu hizo zilikuwa sala ya bao 1-1 huku Wakushi wakiaza kupata bao dakika 9 kupitia kwa Richard anayecheza kikosi cha Mtibwa Bm dakika ya 34 Nughutu walichomoa bao hilo kupitia kwa Denes Raia wa Ghana.

 

Na radhimika kutaja jina Moja Moja kwa vile Mwamuzi wa hakika alimpatia karatasi iliyoandikwa jina moja moja kwa kila timu,alipoulizwa Mwamuzi huyo alisema hiyo ni Michuano ya Ndondo.

 

Kipindi cha Pili Vijana wa Wakushi waliingia kwa kasi ya ajabu ambapo dakika 72 Richard tena alifunga bao la Pili kabla ya Gira kupachia bao la 3 dakika ya 86 ambapo baada ya kufunga bao hilo alikimbilia kwa mashabiki wa Nughutu na kushangilia kwa style ya Mghana wa Simba Bernard Morrison ikiwa ni fumbo kwa mashabiki hao waliotamba kuwa na wachezaji raia wa Ghana.

 

Uchunguzi uliofanywa na Mtandao huu umebaini kwamba timu hiyo kweli iliwachezesha wachezaji watatu raia wa nchini Ghana.

No comments:

Post a Comment

MUUZA MAGAZETI ADAIWA KUJINYONGA MUDA MFUPI BAADA YA KUTOKA KWENYE KIKAO CHA MAZISHI YA DADA’KE.

                            Pili Sebuge Mama mzazi wa marehemu . ....Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa Ngoma B Rehema Matonya ...Miili ya m...