Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Tuesday, August 17, 2021

DIAMOND PLATNUMS NA KUNDI LAKE LA WASAFI WALIVYOTINGA SOKO LA KINGALU MOROGORO.

Ustaa ni noma Mkubwa Fella mwenye Kapero Pausa kwenye Kidali cha nguvu na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro na  Mbunge wa Jimbo la Morogoro kwa pamoja wakisubiri Msanii Nassib Abdul /Diamond Platnums ashuke kwenye gari wamlaki 
                        ,,,,,,Diamond akishuka kwenye gari


....Diamond akielekea kwenye Vibanda vipya  vya wamachinga walivyojengw akwe  kwenye Viwanja wa Soko hilo


Mitaa ya Vibanda hiyvo imepewa majina ya Viongozi wa kitaifa ambapo Diamond alikatia Mtaa wa Makamo wa Rais Mh Mpango
SIMBA  wa Morogoro Seleman Msindi Afande Sele anaye alikuwepo kwenye Msafara huo
Mh Aziz Abood kushoto akiwa na Diamond[kulia Kati ni Chief Kingalu
Nyomi ya watu liyofurika kwa dakika 15 baada ya kupata taarifa kwamba Diamond anatinga kwenye Soko hilo
         Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Albert Msando,
        Chief Kingalu  ambaye soko hilo limepewa jina lake

 Mkuu wa Wilaya ya Morogoro akizungumza kwenye hafla hiyo mwenye nguo za karoti kulia ni Diamond.

Kushoto mwenye Flana ya Mistari  ni Mbunge wa jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood na mwenye kofia nyeusi  ni Chief wa kabira la Waluguru Chief Kingalu 

Diwani wa Kata ya Mji Mpkuu lililpo soko hilo Mh Hassan Malingo[kulia] akimpa maelezo Mwandishi wa Mtandao huuKati] kuhusiana na Soko hilo. kuhsoto ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wapiga Picha Mkoa wa Morogoro  Marekani Vjovu 
Soko Kuu la kisasa la Mkoa wa Moorogoro 'Soko la Chief Kingalu'

 TASWIRA.


 

Na Dunstan Shekidele.Morogoro.

 

BIG Boss wa kundi la Wasafi Nassib Abdul ‘Diamond Platnums’ Wiki iliyopita alitinga Soko kuu la Morogoro Maarufu Soko la Chief Kingalu na kutembelea vibanda vipya vya Wamachinga vilivyojengwa nje ya Soko hilo la kisasa.

 

Diamond na kundi zima la Wasafi wakiongozwa na wenyeji wao wasanii wa Morogoro mkongwe Seleman Msindi’Afande Sele’na Bell 9 walifika mkoani Morogoro kwa lengo la kwenda kupiga show kijiji cha Kiloka Jimbo la Morogoro Kusini linaloongozwa na Mbunge Hamis Tale tale ‘Babu Tale’ ambaye pia ni Meneja  mkuu wa Diamond na kundi hilo la Wasafi.

 

Kijiji hicho cha Kiloka kipo takribani kilomita 20 kutoka Morogoro mjini hivyo kundi  la Wasafi likiwa njiani kuelekea kijijini hapo walikatiza Soko la Kingalu na kutembelea vibanda hivyo vya wamachinga.

 

Akiwa sokoni hapo Diamond na kundi lake walipokewa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mh Albert Msando, Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Mh Aziz Abood na Chief wa 15 wa kabira la Waluguru ambaye Soko hilo linalomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro lilipewa jina lake kwa agizo la Rais wa awamu ya 5 Hayati John Pombe Magufuli

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...