Shekidele Blogs

Shekidele Blogs
Karibuni sana wadau wa blog ya Shekidele kwa mawasiliano zaidi 0715 28 90 73

Monday, July 19, 2021

YARIYOJIRI KUMBI ZA STAREHE MWISHONI MWA WIKI, MTU ANAYESHUKIWA KUWA NI ASKARI AVAMIA WANENGUAJI WA BENDI YA MAISHA MAPYA AKIWA NA SIMU YA UPEPO.


                       ..... Yahya Masauti katika Ubora wake


                           ....Wakisebeneka kwa Style ya Saluti
Jamaa huyo akilisakata Sebene kwa style ya kushika kichwa huku baadhi ya wanenguagi wakimkodolea macho

Mnenguaji ingizo jipya ya band hiyo kutoka FM Academia akifanya yake juzi
...Mnenguaji ingizo jipya kutoka Extra Bongo ya jijini Dar akiwapagawisha mashabiki
Prezedaa wa band hiyo Abubakar Pugi aki Rap kwa lengo la kuwajaza Mzuka wanenguaji hao
...Kiongozi wa band hiyo Joshua Malekela akiwajibika jukwaani


 Yahya Masauti na Kumfuu Style jipendeke ule teke la shingo

 


 

                 Na Mlala Nje Dunstan Shekidele,Morogoro.

JAMAA Mmoja ambaye hakufahamika mara moja anayeshukiwa kuwa ni Afande jumamosi iliyopita aliwashangaza watu baada ya kuwavamia wanenguaji wa band Pendwa ya Maisha Mapya’Full Vipaji’ huku akiwa na simu ya Upepo ‘Radio Call.’

Mara nyingi simu hiyo hutumiwa na baadhi ya vitengo vya Majeshi yote nchini JWTZM, Polisi, Magereza, Uhamiaji, Zima Moto, Mgambo wakiwemo wa kampuni binafsi za ulinzi   na baadhi ya  Mashirika ya Umma na Binafsi.

Kama kawaida Wiki end iliyopita Mlala nje alitinga kwenye ukumbi [jina kapuni] uliopo Mazimbu ambapo Vijana wa   Maisha Mapya waliuwasha moto wa ‘ges’ kwenye kiwanja hicho na Mlala nje alitinga kwa lengo la kusaka Matukio.

Wanenguaji wa Band hiyo yenye Mashabiki wengi Mkoani Morogoro walipoanza kulisakata Sebene Mlala nje aliwa photoa Mapicha Picha  wakicheza Style ya kujirusha hewani kama ‘Nyani.’

Ghafla Jamaa huyo alipanda jukwaani bila kukaribishwa aliiweka chini Radio Call yake na kujichomeka kwenye mstari na kushiriki kusebeneka na wanenguajia hao.

Kwa vile wanenguaji hao walikuwa kikazi zaidi na kamwe huyo hawana ytani kwenye kazi yao,Yahya Masauti aliamua kumkwida jamaa huyo na kumshusha kinguvu jukwaani.

  Njemba hiyo nayo ilikuwa fiti kimazoezi livuta ‘Hand Black’iligima kushuka jukwaani kilazimisha nayo ipigwe picha wakati inakata nyonga.

Baada ya kuona hali ya hewa  imechafuka Kiongozi wa Band hiyo Joshua Malekela Maarufu ’Joshkera Msingis’wa mwisho kulia alimuamulu Yahya kumuacha Jamaa huyo afanya anavyo taka huku wanamuzi hao wakisiticha kucheza wakimkodolea Macho Mgeni huyo aliyeingia nyumba ya watu bira hodi.

Baada ya kususiwa jukwaa Jamaa huyo alimuamulu Mlala Nje ampige Picha na mara baada ya kupigwa Picha aliokota Radio Call yake na kushuka Jukwaani.

Mlala nje alipomaliza kupiga Picha show hiyo alimtafuta  kwa lengo la kuhojiana naye na maswali ya msingi yalikuwa mawili moja kujua anafanya kazi gani pili kwa nini alivamia jukwaani kibabe huku akiwa na Radio Call.

Juhuzi hizo zilikwama kufuatia Mlala nje kumsaka jamaa huyo mkumbi mzima bila mafanikio na baadhi ya watu walipoulizwa walisema  baada ya kushuka jukwaani moja kwa moja alitoka nje ya ukumbi. 

Baadhi ya mashabiki walisikika wakisema huenda jamaa huyo katoloka lindoni kana kupa moja Moto moto baridi  kama tunavyofaamu msimu huu ni wa baridi kali

Baadae Wanenguaji wa Chama hilo la wana linaloundwa na Vijana wadogo waliokomaa Vichwa kwa Ugumu wa Maisha, walisebeneka kwa style ya kupiga saluti

No comments:

Post a Comment

DAKTARI NA MTANGAZAJI WAFUNGUKA MAZITO MADHARA YA MTOTO MCHANGA KUKATISHWA ZIWA LA MAMA.

Somo Farha Abraham akiwa studio za Planet Fm. Daktari Sadick Juma akizungumza na Mwandishi wa habari hizi.     Na Dunstan Shekidele,Moro...