Beki kisiki wa Yanga Dickson Job ambaye amepewa maelekezo na baba yake kuelekea mchezo wa Simba na Yanga julai 25
Dickson Job wakati akiitumikia Mtibwa Sugar ya Manungu Turiani Wilaya ya Mvomero Mkoa Morogoro
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
JOTO la gemu ya watani wa jadi nchini Mabingwa mara 4 mfurulizo Simba yenye Maskani yake Mtaa wa Msimbazi Kariakoo Dar na Mabingwa wa kihistoria Yanga yenye Maskani yake Makutano ya Mitaa ya Jangwani na Twiga Kariakoo linazidi kushika kasi.
Kuelekea kwenye mchezo huo wa fainali ya Kombe la Shirikisho ‘FA CUP’ utakaopigwa Mkoani Kigoma Jumapili ya Julay 25 baba mzazi wa beki wa Yanga Dickson Job amemfunda mwane kuelekea mchezo huo.
Leo asubuhi Mwandishi wa Mtandao huu anayechimba habari za chini ya Kapete alifanikiwa kuzungumza na Nickson Job Maarufu ‘Shukuru’ambaye ni baba mzazi wa beki wa kutumainiwa wa Yanga Dickson Job.
Kwenye Mahojiano hayo Maalumu mzazi huyo alisema mengi ikiwemo historia ya mwanaye toka anazaliwa mpaka sasa ikiitumikia timu hiyo kubwa ya Yanga.
Sitaka kusema mengi Clip video ya mahojiano hayo Part One na Paty Two yataruka hewani hivi Punde kwenye shekidele Online tv.
lfahamike kwamba deki huyo kisiki wa yanba baba yake mdogo ni Yule winga wa zamani wa Simba Nsa Job vile vile kwa wakazi wa Morogoro watamfamu babau wa beki huyo Hayati Mzee Job aliyefariki dunia hivi karibuni na kuzikwa kwao Mkoani Mbeya.
Enzi za uhai wake Hayati Job alikuwa diwani wa miaka Mingi wa Kata ya Mafiga huku Mke wake Mama Job naye akiwa diwani Kata ya Sultan Area.
Mh Job pia alikuwa akimiliki baa Maarufu Mkoani Morogoro ya Chipukizi iliyopo jingo la CCM Wilaya Mtaa wa Makongoro, Mzee Job pia alikuwa shabiki Kindaki ndani wa Man U na kwamba aliweka nadhiri kwamba siku akiaga dunia azikwe na bendera ya Man U anayoimiliki kwa muda mrefu na kweli kwenye mazishi yake walifanya hivyo.
Mwenyezi Mungu ampunzishi Mzee wetu anapostahili huku tukimuomba amsamehe makosa yake.
No comments:
Post a Comment