Mwenyekiti wa Tawi kuu la Yanga Mkoa Morogoro lssa Chabala akiwatumia maneno ya Shombo Mashabiki wa Simba waliovamia tawi hilo mara laa ya timu yao kuinyuka Yanga bao 1-0
Baada ya kutoka tawi la Yanga Mashabiki hao walitinga Mitaa ya Mwembesongo wakiwa na khanga iliyoandikwa Simba Bingwa
Shabiki kindaki ndani wa timu ya Simba ambaye ni Mwanachama wa tawi la Shujaa Morogoro Maarufu Haji Manara ya Morogoro, aliongoza Maandamano hayo akiwa na duraha kama yote ya kumfunga Mtani wao, Shabiki huyo akipozi mbele za Kamera ya Mtandao huu maeneo ya shule ya Msingi Mwembesongo
Na Dunstan Shekidele,Morogoro.
BAADA ya timu yao kulipa kisasi Mashabiki wa Simba wamevamia
tawi kuu la Yanga la Mkoani Morogoro, huku wakiimba nyimbo zinazotaja jina la Mzee Mpili.
Kundi hilo la Mashabiki wa Simba wake kwa waume
Vijana kwa Wazee, Mara baada ya Simba kukata ‘ngebe’ za Mzee Mpili kwenye
mchezo wa fainali ya Michuano ya Azam Federation Cup uliopigwa jana Uwanja wa
Lake Tanganyika Mkoni Kigoma.
Kukamilika kwa
Mnyama Simba kuitandika Yanga bao 1-0,kundi hilo la Mashabiki wa Simba walianza
Maandamano yao yasio na kibali cha Polisi kuanza kwenye tawi kuu la timu hiyo lililopo
Mji Mpya jirani na Soko na kuendelea kwenye tawi kuu la watani zao Yanga
lililopo pia Mji Mpya jirani na Stend ya Daladala wakisema nyinyi mmetupiga
ngumi ya mgongoni ambayo haina Point sisi leo tumewatandika ngumi ya Kichwani
ambayo imetupatia kombe na Pesa.
Licha ya maneno hayo ya ‘Shombo’ waliokwenda
Sambamba na Machungu ya Kufungwa lakini Mashabiki hao wa timu ya Wananchi’Yanga’
walikuwa kimwa wakinywa Tangawizi, kahawa na Kashata.
Huku Mwenyekiti wa Tawi hilo lssa Kitukwa’Maarufu
lssa Chabala’akijibu Mapigo naye akiwakera Mashabiki hao wa Simba akisema “Mwaka
huu tumewapiga Mara mbili Kule Zanzibar na juzi tarehe 3 pake kwa Mkapa, leo tumewachia
ili amani irejea kwenye timu yenu kama tungewafunga Mngemfukuza Haji Manara
mkimshutumu kwamba ana urafiki na bosi wetu GSM tukutane kwenye Ngao ya hisani
mwezi ujao”alisema Mwenyekiti huyo wa tawi kuu la Yanga Mkoani Morogoro.
Baada ya maneno hayo Kundi hilo la Mashabiki wa
Simba liliondoka kwenye tawi hilo Mwandishi wa Mtandao huu aliyeweka kambi
kwenye matawi hao ya Simba na Yanga ambayo yako jirani jirani yakitenganishwa
na mitaa miwili peke wake aliweka Kambi kwenye Matawi hayo akisaka stori za Chini
ya Kapeti.
Baada ya nusu saa ndoka kundi hilo la Simba kuondoka
kwenye tawi hilo la Yanga, ghafla
Mwenyekiti wa Tawi kuu la Simba Mkoani Morogoro ‘Maarufu tawi la Shujaa’ Bw
Saidi Mkwinda alitinga kwenye tawi la Yanga na kumvamia Mwenyekiti wa tawi hiyo
lssa Chabala nini kilitoea endelea kuwa jirani na Mtandao huu muda wote.
No comments:
Post a Comment